Nguza Viking: Waliosamehewa baada ya kufungwa kwa ubakaji Tanzania wamshukuru Magufuli kwa kumwimbia

Wabakaji waliosamehewa wamshukuru kwa kumuimbia Magufuli Haki miliki ya picha AFP
Image caption Magufuli aliwaambia wanafaa kumshukuru Mungu

Rais wa Tanzania John Magufuli Jumanne alikutana na wanamuziki wawili aliowasamehe takriban wiki tatu zilizoita, licha ya kuwa walikuwa wanatumikia kifungo cha maisha jela kwa kuwabaka wasichana 10 wa shule mwaka 2003.

Nguza Viking, anayefahamika pia kama Babu Seya, na mtoto wake Johnson Nguza, ambaye pia anafahamika kama Papii Kocha, walimshukuru Rais Magufuli kwa kuwasamehe ambapo walimwimbia wakati walimtembelea katika Ikulu.

Taarifa ya Ikulu ilimnukuu Magufuli akisema, "Najua mmekuwa mkihangaika kutaka kuniona, nikaona wacha niwasikilize, hata hivyo mshukuruni Mwenyezi Mungu ambaye ndiye hutoa msamaha, sasa nendeni mkachape kazi, na mmtangulize Mungu".

Watetezi wa haki za watoto walikosoa msamaha huo.

Walikuwa wametumikia kifungo cha miaka 13 wakati waliachiliwa kwa kuwabaka wasichana walio kati ya umri wa miaka 6 na 8.

Haki miliki ya picha Ikulu, Tanzania

Wawili hao walikuwa miongoni mwa wafungwa 61 waliopata msamaha wa rais wakati wa hotuba yake ya uhuru.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii