Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 03.01.2018

Philippe Coutinho Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Philippe Coutinho

Mchezaji wa Liverpool Philippe Coutinho anaamini kuwa alicheza mechi yake ya mwisho kwa klabu hiyo lakini itagharimu takriban pauni milioni 133 kuhamia Barcelona mwezi huu. (Times)

Liverpool watamsaini Alexis Sanchez, 29, kutoka Arsenal kwa pauni milioni 40 kuchukua mahala pake Phillippe Coutinho, ikiwa ataondoka Anfield. (Irish Independent)

Meneja wa Arsenal amefungua mlango wa kuuzwa kwa mshambuliaji raia wa Chile Sanchez mwezi huu. (Mirror)

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Alexis Sanchez

Mchezaji wa RB Leipzig Naby Keita anatarajiwa kusalia katika klabu hiyo ya Ujerumani kwa msimu wote wakati kiunga huyo wa kati raia wa Guinea, anasubiri hadi msimu ujao kuweza kuhamia Liverpool kwa kima cha pauni milioni 55. (Bild kupitia Liverpool Echo)

Klabu hiyo ya Ujerumani pia imesema kuwa kumuuza mshambuliaji Timo Werner, ambaye amehusishwa na Real Madrid na Bayern Munich haiko katika mipango yao. (AS)

Chelsea wako tarayi kuafikia pauni milioni 50 kwa beki wa Juventus mbrazil Alex Sandro, 26. (Mirror)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Alex Sandro

Lakini meneja wa Chelsea Antonio Conte ametuliza uvumi kuhusu kununuliwa kwa mlinzi wa Juventus Giorgio Chiellini 33, mwezi Januari. (Daily Mail)

Conte pia amesemamlinzi mbrazil David Luiz, 30, na mbelgiji Michy Batshuayi, 24, wanaweza kuondoka Stamford Bridge mwezi Januari ikiwa wangependa kufanya hivyo. (Telegraph)

Fenerbahce watatoa ofa kwa mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud, 31, mwezi huu. Ripoti nchini Uturuki zinasema kuwa klabu hiyo ina mpango kumsaini kuchukua mahala pake Robin Van Persie. (Fanatik kupitia Football London)

Mada zinazohusiana