Watu wanakufa wakati wa upasuaji Afrika

Madaktari wakiwa katika upasuaji
Image caption Madaktari wakiwa katika upasuaji

Wanasayansi wamebaini kuwa vifo vinavyotokana na kufanyiwa upasuaji kwa wagonjwa barani Afrika ni mara mbili zaidi ya takwimu za wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji katika nchi nyingine duniani,hiyo ikiwa ni matokeo ya usimamizi mbovu wa shughuli za upasuaji na ukosefu wa vifaa vya hospitali na wataalam.

Utafiti wa kisayansi umegundua kuwa umri wa wagonjwa wanaokufa wakati wakifanyiwa upasuaji kwa Afrika ni mdogo zaidi na wanakuwa na afya njema ikilinganishwa na wale ambao hufa wakati wa upasuaji katika mataifa mengine duniani.

Utafiti huo umegundua pia kuwa idadi ya upasuaji ni mdogo mara ishirini ikilinganishwa na mahitaji halisi ya upasuaji unaohitajika katika nchi za Afrika.Ripoti ya utafiti huo imechapishwa katika jarida la kitabibu la Lancet.