Mapacha waliounganaTanzania wamepelekwa kwa uchunguzi wa kiafya
Huwezi kusikiliza tena

Mapacha waliounganaTanzania wamepelekwa kwa uchunguzi zaidi wa kiafya

Mapacha walioungana Maria na Consolata ambao kwa sasa wanasoma chuo kikuu cha RUCO mkoani Iringa kusini magharibi mwa Tanzania,wamepelekwa katika hospitali ya taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam nchini Tanzania ,kwa uchunguzi zaidi wa kiafya.

BBC iliwahi kuwatembelea mapacha hao wakati wakijiandaa na mitihani yao ya kidato cha sita shule ya sekondari ya udizungwa mkoani humo,ambapo waliweka wazi mipango yao ya baadaye wakiwa katika hali hiyo hiyo huku wakiwa ni wenye furaha na afya njema.

Anna Nkinda ni afisa uhusiano wa taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete,anaelezea walivyowapokea mapacha hao.