Treni yagonga lori na kushika moto Afrika Kusini

Scene of train crash Haki miliki ya picha @ER24EMS
Image caption Lori lilikosa kusimama katika makutano ya barabara na reli

Treni ya kubeba abiria imeshika moto baada ya kugongana na lori nchini Afrika Kusini.

Maafis awanasema watu 12 wamefariki na wengine 268 kujeruhiwa.

Ukanda wa video umeonesha behewa moja la treni hiyo likiwa linawaka moja, pembeni kukiwa na gari lililopondwa pamoja na lori lililopinduka.

Abira ambao waliokolewa kwenye treni hiyo walikuwa pembeni na mizigo yao wakiwa wamekwama.

Ajali hiyo ilitokea karibu na mji wa Kroonstad katika jimbo la Free State baada ya lori kukosa kusimama katika makutano ya barabara na reli.

Haki miliki ya picha @ER24EMS
Image caption Baadhi ya abiria walinusurika bila majeraha

Polisi wamenukuliwa wakisema abiria 850 wameondolewa kutoka kwenye treni hiyo wakiwa salama.

Mada zinazohusiana