Tunayoyafahamu kuhusu simu 'nyekundu na kijani' zilizotumika na nchi za Korea Kusini na Kaskazini

Hii ni simu inayounganisha Korea Kusini na Kaskazini katika nyumba ya uhuru Korea Kusini. Upande wa pili wa Korea Kaskazini ina simu kama hii Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Hii ni simu inayounganisha Korea Kusini na Kaskazini katika nyumba ya uhuru Korea Kusini. Upande wa pili wa Korea Kaskazini ina simu kama hii

Kila siku kwa miaka miwili, afisa wa Korea Kusini amechukua simu yenye rangi ya kijani na kumpigia afisa mwenzake upande wa pili , nje tu ya mpaka wa Korea Kaskazini. Lakini hamna aliyejibu simu hiyo.

Hayo yote yakabadilika saa 9.30 ( 6.30 saa za GMT) tarehe 3 Januari 2018. Katika muda wa dakika 20,pande zote mbili walitumia laini zao wakiwa na matumaini ya kupungunza ugomvi baina ya nchi zao za Korea.

Simu hiyo ipo katika kijiji cha mpaka wa Panmunjom, ambapo pamekuwa chanzo cha mawasiliano baina ya majirani hao ambao kimsingi bado wako vitani. Lakini tunafahamu nini kuhusu simu hiyo?

'Hamna Utani'

Ni jambo linalokaa kama limetoka moja kwa moja katika nyakati za vita vya baridi - ni kweli. Likijengwa kwenye dawati mbalo ziliwekwa simu zenye rangi ya kijani na nyekunde pamoja na kompyuta, laini ya Kusini na Kaskazani ilizinduliwa mwaka 1971 kwa minajili ya mawasiliano kati ya shiriki la msalaba mwekundu wa Korea Kaskazani na Korea Kusini.

Laini za ziada zilizinduliwa mwaka 1972 wakati wa maongezi kuhusu kuunganishwa kwa nchi hizo mbili tena mwaka 1990 na 2000

Hii leo kuna takribani laini 33 kati ya korea hizi mbili, tano kati yake ni kwa ajili ya mawasiliano ya kila siku, 21 ni kwa ajili ya mazungumzo baina yao korea, 2 ni kwa ajili ya maswala ya anga, mbili kwa ajili ya maswala usafiri majini na tatu kwa ajili ya mashirikiano ya kuichumi na kibiashara

Lakini zimekuwa hazifanyi kazi tangu mwezi wa pili 2016 wakati Korea ya kaskazini ilipovunja mahusiano na kusini baada ya Seoul kusitisha mradi wa ushirika wa kiuchumi wa Kaesong Industrial Complex baada ya Pyongyang kufanya jaribio ya lanyuklia

Afisa wa zamani wa mawasiliano wa Korea ya Kusini aliueleza mtandao wa habari wa Yanhap namna mazingira ya kazi yalivyokuwa huko mwanzoni mwa miaka ya 1990

'' Simu zote zilikuwa za kazi hatukuweza kuzungumza mengine ama kutaniana'' Kim Yeon -Cheol aliuambia mtandao huo mwaka 2008 kwa kuelezea ratiba ya kila siku ambapo simu zilipigwa kila saa tatu asubuhi na saa kumi jioni kabla ya siku kuisha.

''Sisi tuliwapigia kwenye tarehe zenye namba witiri na na wao walitupigia kwenye tarehe zenye namba shufwa'' aliongeza

hakuna tarehe za namba shufwa ama witiri tena, msemaji wa wizara ya muungano aliiambia BBC, lakini utaratibu wa kupiga simu mara mbili kwa siku umeendelea kwa watu wa korea ya kusini,wanapiga kwenye simu ya kijani.

Simu nyekundu ni ya kupokelea simu kutoka korea ya kusini lakini hakujawa na mwitikio kwa miaka miwili ''kiufundi simu hizi bado zilikuwa zimeunganishwa lakini korea ya kaskazini walikuwa hawapokei simu'' alieleza msemaji huyo

kabla ya mwaka 2016 mwezi wa pili pande hizi mbili zilikuwa zinawasiliana kila siku kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa kila upande ungepiga saa tatu asubuhi kuona kama simu bado zilikuwa zinafanya kazi

''kama tulikuwa na Ujumbe tunge wauliza kaskazini kama wangependa kuupokea na hapo simu ingekatwa na ujumbe ungetumwa ama kwa faksi au kupelekwa ana kwa ana''

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Will the North Koreans be at the Winter Olympics in Pyeongchang next month?

Majira yalivurugwa kidogo mwaka 2015 wakati korea ya kaskazini iliposogeza mbele kwa dakika 30 majira yake

Mazungumzo thabiti

Maamuzi ya Kaskazini kufungua tena mawasiliano haya yalikuja baada ya Kim Jong- un kusema wakati wa hotuba yake ya mwaka mpya mazungumzo yafunguliwe na Seoul na timu yao ishiriki katika michezo Olimpiki katika majira ya baridi korea kusini

Ri Son-gwon anayeiongoza Kaskazini katika mashirikiano haya ya korea anasema Kim Jong -un ametoa amari mawasiliano yafunguliwe tena kujadiliana ''ni wakati sahihi kwa mazungumzo na niwakati sahihi kutuma wawakilishi katika michuano hiyo ya olimpiki ya majira ya baridi (Pyeongchang Winter Olympics)".

Anasema watafanya mawasiliano kwa karibu sana kwa njia ya uwazi na uaminifu na kujadili mazingira ya kufanya kazi na maswala mengine yanayohusiana na kutumwa kwa kikosi chao katika michezo hiyo

Msemaji wa idara ya mawasiliano ya muungano ali iambia BBC simu iliyopigwa jumatano ilikuwa ni kujaribu iwapo bado simu hizo zina fanya kazi,bado ni vigumu kueleza namna mawasiliano hayo yatakavyo endelea ''inaweza kuwa kupitia mikutano ya ana kwa ana au kwa kubadlishana barua'' alisema