Polisi wamshikilia Muisrael anayeuza viungo vya binaadam Cyprus

Moshe Harel anatajwa kuwa na ushirikiano wa karibu na wafanya biashara wakubwa wa viungo vya binadam Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Moshe Harel anatajwa kuwa na ushirikiano wa karibu na wafanya biashara wakubwa wa viungo vya binadam

Polisi nchini Cyprus wanasema wanamshikilia raia mmoja wa Israel anayetuhumiwa kufanya biashara ya viungo vya binadam.

Moshe Harel amehusishwa kufanya biashara ya figo kwa matariji wa Israel takriban miaka kumi sasa.

Amehusishwa kuchukua figo za raia wa Kosovo pamoja na Uturuki na nchi nyingine kadhaa ambao mpaka sasa hajawalipa chochote.

Msemaji wa polisi nchini Cyprus amesema mtu huyo alikamatwa uwanja wa ndege wa Larnaca mwezi Desemba.

Anatarajiwa kufikishwa mahakamani siku ya Jumanne kujibu mashtaka yanayomkabili.

Anahitajika kwa makosa kama hayo nchini Kosovo.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii