Mawaziri wawili wa zamani wakamatwa kwa tuhuma za rushwa Zimbabwe

Walter Mzembi aliyekuwa waziri wa mambo ya nje amesema tuhuma hizi ni za kisiasa
Image caption Walter Mzembi aliyekuwa waziri wa mambo ya nje amesema tuhuma hizi ni za kisiasa

Mawaziri wawili wa zamani wa Zimbabwe wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za rushwa.

Samuel Undenge ambaye alikua waziri wa nishati anatuhumiwa kutumia dola elfu kumi na mbili kwa kampuni ambayo haukufanya lolote.

Kwa upande wa wake Walter Mzembi aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wakati wa utawala wa Robert Mugabe aliyeondolewa madarakani mwezi Novemba, anatuhumiwa kuchangia baadhi ya mali za televisheni ya Taifa kwa kanisa moja nchini humo bila ya idhini ya serikali.

Image caption Waziri wa zamani wa nishati Samuel Undenge

Wote wawili wamekana mashitaka hayo.Inatarajiwa kesi hizo zitasikilizwa tena baadae mwezi huu.

Rais mpya Emmerson Mnangagwa ameapa kupambana na rushwa iliyodumu karibia wakati wote wa utawala wa Robert Mugabe.

Mnangagwa aomba Zimbabwe iondolewe vikwazo

Wakuu wa jeshi wateuliwa kuwa mawaziri Zimbabwe

Lakini wakosoaji wanasema watu wanaokamatwa na kufikishwa mahakamani ni wale tu wanaohoji namna Mnangagwa aliyoingia madarakani.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii