Polisi Misri wapambana na waandamani kutokana na kifo cha kijana mmoja

Waandamanaji wakichoma maeneo yanayozunguka kituo cha polisi Cairo
Image caption Waandamanaji wakichoma maeneo yanayozunguka kituo cha polisi Cairo

Mapigano yameripotiwa kati ya vikosi vya polisi na waandamanaji nje ya kituo cha polisi mjini Cairo kutokana na kifo cha kijana mmoja aliyekuwa rumande.

Taarifa zinasema kuwa waandamanaji hao wanaishutumu polisi kwa kumtesa mpaka kusababisha kifo cha kijana huyo.

Wamechoma magari ya polisi, kuyapiga mawe na kujaribu kuchoma pia kituo cha pilisi.

Polisi wametumia mabomu ya kutoa machozi na kuwakamata baadhi ya waandamanaji.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Maandamano hayo yamepelekea kujeruhiwa kwa watu kadhaa

Kijana huyo aliyefahamika kwa jina moja la Afroto alikamatwa siku ya Ijumaa kwa tuhuma za kujihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya na polisi inasema alifariki baada ya kupigana na wafungwa wenzake.

Hali ya utulivu ilirejea katika mji wa Cairo baada ya mkuu wa polisi kuahidi kufanyai upelelezi suala hilo.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii