Barcelona yamnunua Philippe Coutinho kwa pauni milioni 142

Philippe Coutinho in action for Liverpool Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Barcelona yamnunua Coutinho kwa pauni milioni 142

Barcelona imemsaini kiungo wa kati wa Liverpool Philippe Coutinho kwa pauni milioni 142, ikiwa ni moja na mauzo ghali zaidi kuwai kufanywa.

Liverpool watapata malipo ya mapema ya pauni milioni 105 kwa mbrazili huyo kwa miaka 25 huku pesa ambazo zitasalia zikitarajiwa kulipwa baadaye.

Coutinho atasaini mkataba wa miaka mitano huko Nou Camp.

Alijiunga na Liverpool akitokea Inter Milan kwa pauni milioni 8.5 mwezi Januari mwaka 2013.

Pesa alizonunuliwa Coputnho ziko chini ya pauni milioni 200 ambazo Paris St-Germain iliwalipa Barcelona kumnunua Neymar na pauni milioni 165.7 ambazo itagharimu PSG kumununua Kylian Mbappe baada ya kumaliza mkopo wake huko Monaco.

Mauzo ghali zaidi ya wachezaji duniani

£200m - Neymar (Barcelona kwenda Paris St-Germain) 2017

£165.7m - *Kylian Mbappe (Monaco kwenda PSG kwa mkopo akiwa huru kununuliwa) 2017

£142m - Philippe Coutinho (Liverpool kwenda Barcelona) 2018

£135.5m - Ousmane Dembele (Borussia Dortmund kwenda Barcelona) 2017

£89m - Paul Pogba (Juventus kwenda Manchester United) 2016

Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Alijiunga na Liverpool akitokea Inter Milan kwa pauni milioni 8.5 mwezi Januari mwaka 2013.

Mada zinazohusiana