Urusi yatibua shambulizi la ndege isiyo na rubani kwenye kambi yake ya jeshi Syria

The damaged tail of a jet. Anonymous photo via Roman Saponkov Haki miliki ya picha Roman Saponkov
Image caption Mwandishi wa habari wa jeshi la Urusi alichapisha picha katika mitandao ya kijamii zilizoonekana kuonyesha ndege zilizoharibiwa

Vikosi vya Urusi vimetibua shambulizi la kutumia ndege isiyo na rubani kwenye kambi ya jeshi la wanahewa nchini Syria siku chache baada ya ripoti kuwa maroketi ya waasi yaliharibu ndege kadha.

Jaribio la kushambulia uwanja wa ndege wa Hmeimim karibu na mji wa kaskazini magharibu wa Latakia siku ya Jumosi zilitibuka wakati ndege isiyo na rubani ilidunguliwa.

Wanajeshi wawili wa Urusi waliuawa wakati kambi hiyo ilishambuliwa tarehe 31 Disemba.

Kambi hiyo ya Hmeimim ndiyo kiunga muhimu kwa vita vya Urusi nchini Urusi

Haki miliki ya picha Roman Saponkov
Image caption Mwandishi wa habari wa jeshi la Urusi alichapisha picha katika mitandao ya kijamii zilizoonekana kuonyesha ndege zilizoharibiwa

Hakuna maafa ya uharibifu kwenye kambi hiyo ulioripotiwa hadi sasa.

Ndege hiyo iliripotiwa kuwa na injini iliyofungwa kwennye mbao ambayo ilikuwa imefungiwa vilipuzi viwili vya kujitengenezea.

Urusi bado hajatamka lolote kuhusu ripoti hizo.

Wiki iliyopita mwandishi wa habari wa jeshi la Urusi Roman Saponkov, alichapisha picha katika mitandao ya kijamii zilizoonekana kuonyesha ndege zilizoharibiwa kwenye shambulizi la roketi katika kambi ya Urusi Hmeimim tarehe 31 Disemba.

Haki miliki ya picha Roman Saponkov
Image caption Mwandishi wa habari wa jeshi la Urusi alichapisha picha katika mitandao ya kijamii zilizoonekana kuonyesha ndege zilizoharibiwa

Mada zinazohusiana