Misri;Ahmed Shafik kutowania tena Urais mwaka huu

Waziri mkuu wa zamani wa misri Ahmed Shafik Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waziri mkuu wa zamani wa misri Ahmed Shafik

Waziri mkuu wa zamani wa misri Ahmed Shafik, amesema kuwa hatoshiriki kama mgombea wa kiti cha uraisi mwaka huu 2018.

Katika ukurasa wake wa twitter aliandika kuwa ameona kuwa yeye si mtu sahihi kuongoza nchi katika kipindi kijacho.

Shafik ndie alikua kionekana kuwa mpinzani mwenye nguvu kwa rais Abdel Fattah al-Sisi katika uchaguzi utakofanyika mwezi machi mwaka huu.

Waziri mkuu huyo wa zamani awali alitangaza nia yake ya kugombea urais akiwa falme ya kiarabu, muda mfupi baada ya kutangaza nia yake hiyo, mamlaka za uarubuni walimrudisha misri, ambapo hakuonekana kwa muda na baadae akaonekana na kukanusha madai ya kutekwa.

Wachambuzi wa siasa za misri wanasema kuwa kutokana na mfululizo wa matukio yanahusianishwa na kugombea kwake , bado watu wanabaki kujiuliza ni sababu gani hasa iliyomfanya ajiote katika kinyang'anyiro cha uarisi.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii