Kitabu cha Fire and Fury kufafanuliwa na mtunzi

Steve Bannon Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Steve Bannon

Donald trump amemshambulia mwandishi aliemuelezea kama kiongozi asiye na msimamo na kudai kuwa kitabu cha Michael Wolf ni cha kutungwa tu.

''naona ni kama hadithi ya kutungwa tuu, na ni aibu mtu anaweza fanya kitendo kama hicho. Sheria za kashfa za uongo nchi hii ni dhaifu sana, zingekua na nguvu hii ingesaidia sana. Vitu kama hivi visingetokea ambapo mtu anaongea tuu chochote kinachomjia kichwani kwake. Hajawahi kunifanyia mahojiano kabisa katika ikulu ya white house, sijawahi kuwa na mahojiano naye, "Trump aeleza.

Wakati huo huo aliyekuwa msaidizi wa mipango wa rais trump, Steve Bannon amefafanua maelezo aliyoyatoa katika kitabu chake kuhusu mwenendo wa urais wa Trump.

Katika kitabu hicho kinachoitwa Fire and Fury, Bannon anaelezea juu ya mkutano kati ya mtoto wa Trump na kundi la warusi kuwa haukua wa kizalendo.

Bannon anasema yeye alimlenga kiongozi wa zamani wa kampeni Paul Manafort na sio mtoto wa trump.

Na kumuelezea mtoto wa trump kuwa ni mtu mzuri na mzalendo.

Mada zinazohusiana