Walio katika ndoa za ''njoo tuishi'' kuadhibiwa Burundi
Huwezi kusikiliza tena

Walio katika ndoa za ''njoo tuishi'' kuadhibiwa Burundi

Serikali ya Burundi imesema inajiandaa kuwaadhibu watu ambao wanaishi katika mahusiano ya mume na mke lakini wamekaidi amri ya kufunga ndoa.

Hii ni baada ya muda uliotolewa mwaka jana kumalizika. Burundi ilichukua hatua hiyo kwa hoja ya kudhibiti ongezeko la watu na kusimamia maadili mema.

Kutoka Bujumbura, mwandishi wetu Ramadhani KIBUGA anaarifu zaidi.