Mchunguzi maalum Robert Mueller afanya mazungumzo ya kumhoji rais Trump

Rais Donald Trump huenda akahojiwa na Robert Mueller Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rais Donald Trump huenda akahojiwa na Robert Mueller

Mawakili wa Donald Trump wako katika mazungumzo na wachunguzi ambao wanataka kumhoji rais wa Marekani ikiwa ni miongoni mwa uchunguzi wa idara ya haki, kulingana na ripoti.

Gazeti la The Washington Post, likinukuu duru iliokaribu na rais Trump limesema kuwa kiongozi wa uchunguzi huo Robert Mueller huenda akamhoji katika kipindi cha wiki chache zijazo.

Hatahivyo kundi la mawakili wa Trump halijathibitisha ripoti hizo.

Bwana Mueller anachunguza ushirikiano kati ya kundi la kampeni za bwana Trump na Urusi wakati wa uchaguzi wa 2016.

Wasiwasi kati ya bwana Mueller , wakili mtaalamu aliyechaguliwa kuchunguza ushirikiano wa Urusi na rais umeongezeka tangu uchunguzi kusababisha mashtaka dhidi ya wanachama kadhaa wa zamani katika kundi la kampeni ya Trump.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mchunguzi maalum Robert Mueller katika mazungumzo ya kumhoji rais Trump

Serikali ya rais Trump imekana kushirikiana na Urusi kuhusu uchaguzi na rais huyo ametaja uchunguzi huo kama vita dhidi yake.

Kulingana na The Post, bwana Mueller alizungumza kuhusu uwezekano wa kumhoji rais huyo katika mkutano na mawakili wake John Dowd na Jay Sekulow baadaye mwezi Disemba.

''Swala hili linafanyika kwa kasi kubwa zaidi bila watu kugundua'', gazeti hilo lilimnukuu mtu mmoja aliye karibu na rais ambaye alificha jina lake.

Mawakili wa rais Trump hawataki kumruhusu kuketi chini kwa mahojiano na sasa wanajadiliana iwapo wamruhusu kutoa majibu yalioandikwa kwa baadhi ya maswali kulingana na The Washington Post na NBC.

Kulingana na NBC ambalo liliwahoji watu watatu walio karibu na habari hiyo mazungumzo hayo ni ya awali na yanenedelea.

Kundi la mawakili wa rais Trump hawakuthibitisha ripoti hizo, lakini liliambia vyombo vyote vya habari kwamba Ikulu ya Whitehouse bado inaendelea kushirikiana na mchunguzi huyo.

Mada zinazohusiana