Milio ya risasi yarindima Ivory coast

Sauti za risasi na silaha nzito zimesikika katika mji wa pili kwa ukubwa nchini Ivory Coast, Bouake.
Image caption Sauti za risasi na silaha nzito zimesikika katika mji wa pili kwa ukubwa nchini Ivory Coast, Bouake.

Sauti za risasi na silaha nzito zimesikika katika mji wa pili kwa ukubwa nchini Ivory Coast, Bouake.

Mapigano yamezuka karibu na eneo la jeshi, huku vikundi vya waasi wa jeshi wakihusishwa na tukio hilo.

Mji huo ulikua sehemu ya maandamano mwaka jana kutokana na madai ya kuongezwa kwa mshahara kwa wanajeshi hao.

Katika siku za karibuni, waasi wa jeshi wamekua katika mgogoro na jeshi, wakishutumu kuchunguzwa na kutaka wanachama wake kuondoka mji wa Bouake.

Waasi hao walikua miongoni mwa kikundi cha waasi kilichothibiti eneo la kaskazini mwa Ivory coast kwa karibu muongo mmoja.