Uchumi wa dunia unatarajiwa kuimarika zaidi mwaka huu

WB Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rais wa benki ya dunia Jim Yong Kim

Benki ya dunia imetoa ripoti inayosema kuwa uchumi wa dunia unatarajiwa kuimarika na kukua kwa mwaka huu, baada ya kuwa na matokeo mazuri kuliko ilivyotarajiwa mwaka 2017.

Katika tathmini yake ya kawaida kwa mwaka ulioanza utaongezeka kwa asilimia 3.1, Benki kuu ya dunia imesema kuwa itakua ya kwanza kwa uchumi kufikia malengo yake tangu kudorora kwa uchumi mwaka 2008. Lakini rais wa benki hiyo ya dunia Jim Yong Kim ametoa onyo kuhusu uwekezaji hafifu na nguvu kazi .

Ripoti hiyo inaonesha vigezo hivyo kama ni hatari katika hatua zilizopigwa katika kupunguza umaskini na hali nzuri ya kuishi.

Lakini pia moja ya Mwandishi wa ripoti hiyo anatoa onyo kuwa maendeleo yanaweza kuongezeka au kupungua pia.

Mada zinazohusiana