Sri Lanka yaondoa marufuku ya wanawake kunywa pombe

A Sri Lankan woman holds a cocktail during a drinks competition in Colombo, 26 February 2017 Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wengi wa wanawake Sri Lanka hutazama unywaji pombe kama kinyume na utamaduni wa taifa hilo

Sri Lanka imewaruhusu wanawake waliotimiza umri wa miaka 18 kununua pombe kwa mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya miaka 60.

Serikali imesema itafanyia marekebisho sheria ya mwaka 1955 ambayo ilikiri kwamba imekuwa ikiwabagua wanawake.

Marekebisho hayo ya sheria, ambayo yalitangazwa Jumatano, yana maana kwamba wanawake wataruhusiwa sasa kufanya kazi katika maduka na vituo vya kuuzia pombe bila kuhitajika kuwa na idhini ya awali.

Ingawa sheria ya awali haikuwa inatekelezwa kikamilifu, wengi wa wanawake Sri Lanka wamefurahia mabadiliko hayo.

Wanawake wamekuwa wakishukuru serikali kwenye mitandao ya kijamii.

Kwenye sheria mpya iliyotangazwa na waziri wa fedha Mangala Samaraweera wanawake hawatahitaji idhini kutoka kwa kamishna wa forodha kufanya kazi au kunywa pombe katika maeneo yaliyoidhinishwa, ikiwa ni pamoja na migahawa na baa.

Ingawa wengi wameifurahia, kunao walio na wasiwasi kwamba huenda ikawafanya wanawake kuwa waraibu wa unywaji pombe.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii