Ni kipi vipimo vya afya vya Trump vitafichua?

Trump

Donald Trump atafanyiwa uchunguzi wake wa kiafya wa kwanza akiwa rais Ijumaa - ni kipi anakitarajia?

Wakati Trump anatafika katika kituo cha afya cha Walter Reed Medical Center huko Bethesda, Maryland, atakuwa na habari nzuri na mbaya kwa daktari wake.

Kwanza, zile nzuri.

Hakunywi pombe, na hajawai. Anasema alijifunza kutoka kwa ndugu yake mkubwa Fred ambaye alifariki dunia akiwa na miaka 4.

Pia havuti sigara, "ninawatazama watu wakivuta sigara, alisema mwaka 2015. ni kitu cha kutisha kwangu.

Sasa pia kuna habari mbaya.

Kitabu cha hivi punde kilifichua kuwa chakula kikuu cha Bw Trump ni pamoja na

  • McDonald's
  • Kentucky Fried Chicken
  • Pizza
  • Na Diet Coke

Kulingana na kitabu kilichoandikwa na Corey Lewandowski chakula cha jion cha Tumo kina kalori 2430. Kalori ambazo mwanamume anastahili kula kwa siku ni 2,500.

Afya ya Donald Trump

71

Miaka

  • futi 6 inchi 3 Kimo

  • kilo 107 Uzani

  • 29.5 Makadirio ya kimo na uzito (yanaonyesha uzito ya juu)

  • kilo 6 - 9 Uzani ambao alisema mwaka 2016 angependa kupoteza

Win McNamee/Getty Images

Pia Trump anaonekana kutotilia maanani mazoezi, licha ya yeye kucheza gofu.

Anaamini kuwa mwili wa binadamu ni kama betri ulio na nguvu zinazoweza kumalizwa na mazoezi.

Mwezi Septemba mwaka 2016 - miezi miwili kabla ya uchaguzi alitoa rekodi zake za afya,

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Donald Trump akisubiri chakula chake wakati wa kampeni huko Philadelphia

Kwa juma mafuta yake kwa mwili yalikuwa 169, lakini vipimo vyovyote chini ya 200 si jambo baya.

mpiga wake wa damu ulikuwa 116/70 ambavyo ni viwango vizuri huku ini lake nalo likiwa katika hali nzuri.

Kwa ufupi daktari wake Harold Bornstein, aliandika kuwa Trump alikuwa katika hali nzuri ya afya.

Licha ya afya ya akili ya Tump kutiliwa shaka, vipimo vya leo haviwezi kuhusu hali yake ya kiakili.

Awali Trump alikuwa amejieleza kuwa mtu mwerefu sana.

Trumo ahitaji kutanga hadharani matokeo yake ya kiafya lakini msemaji wake alisema kuwa daktari wa White Hosue Ronny Jackson, atayasoma

Dr Jackson alitoa taarifa ya kurasa mbili baada ya vipimo vya mwisho vya rais Obama mwezi Machi mwaka 2016.