Mkuu wa genge la Yakuza la Japan akamatwa Thailand

Thai policemen with Mr Shirai, displaying the tattoos on his body Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mkuu wa genge la Yakuza la Japan akamatwa Thailand

Polisi wamekamata mkuu wa genge la Yakuza la nchini Jopan ambaye amekuwa mafichoni kwa miaka 15 baada ya picha za chale zake (tattoo) kusamba katika mtadao wa Facebook.

Shigeharu Shirai analaumiwa kwa kumuua mshindan wake kwenye genge hilo mwaka 2003.

Picha za mtoro huyo wa umri wa miaka 74 zilichukuliwa na mtu mmoja nchini Thailand ambaye hakufahamu yeye ni nani.

Magenge ya Yakuza yamekuwa miongoni mwa jamii nchini Japan kwa karne kadhaa na wanakadiriwa kuwa na wanachama 60,000.

Licha magenge hayo kutokuwa haramu, asilimia kubwa ya pesa zao hutokana na kucheza kamari, ukahaba, ulanguzi wa madawa ya kulevya na udukuzi wa mitandao.

Wakati picha hizo zilisambaa mitandaoni, zilivutia polisi wa Japan walioombaa akamatwe.

Polisi walimkamata kwenye mji wa Lopduri kaskanizi mwa Bangkok na atasafirishwa kwenda Japan kukabiliana na mashtaka ya mauaji.

Kulingana na polisi nchini Thailand, alikiri kuwa yeye ni mwanachama wa Yakuza lakini hakukiri kuwa alihusika kwenye mauaji ya mwaka 2003. Alitorokea Thailand mwaka 2005.

Mada zinazohusiana