Pampu za kukama maziwa na kuyahifadhi mwanamke akiwa safarini

Willow breast pumps in use Haki miliki ya picha Willow
Image caption Pampu za kukama maziwa na kuyahifadhi mwanamke akiwa safarini

Kampuni mbili zimetengeneza pampu ambazo zitawasaidia wanawake wanaonyonyesha kukama maziwa na kuyahifadhi wakati wakiwa safarini.

Wanawake wanaotumia pampu kawaida hukama maziwa mara kwa mara kwa siku na kati ya muda wa dakika 20.

Kwa kawaida huunganishwa kwa stima na hutoa sauti.

Kampuni za Willow na Freemie Libert zimetangenezwa kwa njia ambazo zitakuwa rahisi kuvaliwa.

Haki miliki ya picha Freemie
Image caption Pampu za kukama maziwa na kuyahifadhi mwanamke akiwa safarini

Kinyume na za zamani, zasasa hutumia betri na hazina sauti.

Zote ziko kwa maonyesho ya CES ya biashara huko Las Vegas.

Willow ilishinda tuzo kutokana na kifaa hicho kwenye maonyesho ya CES mwaka 2017, kwa sababu pampu hiyo imekuwepo kwa majaribio lakini sasa inaingia rasmi sokoni kwa dola 479.

Hata hivyo imekosolewa mitandaoni kutoka kwa wale wameijaribu wengine wakesema kuwa mifuko hiyo ya maziwa ni midogo mno.

Haki miliki ya picha Willow
Image caption Pampu za kukama maziwa na kuyahifadhi mwanamke akiwa safarini

Mada zinazohusiana