Facebook kufanya mabadiliko makubwa

facebook Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mkurugenzi wa Facebook,Mark Zuckerberg

Mtandao wa kijamii wa Facebook umetangaza kufanya kile inachokiita kuwa ni mabadiliko muhimu ambayo itafawafanya watumiaji wa tovuti hiyo kuwa na mawasiliano yenye umuhimu zaidi katika maisha yao ya kila siku.

Watu watapata habari zaidi juu ya marafiki zao na familia na taarifa juu ya makampuni na taasisi zitapungua kwenye mtandao huo.Mkurugenzi mkuu wa mtandao wa Facebook, Mark Zuckerberg ameeleza kuwa maudhui ya biashara na vyombo vya habari yalikuwa yanamuondoa mtu katika nyakati muhimu ambayo watu wengi wanaithamini zaidi.

Amesema vipaumbele ambavyo Facebook imeviweka ili kuondoa changamoto iliyopo inaweza kumaanisha kuwa watu watatumia muda mfupi zaidi katika mtandao huo ,lakini muda ambao watautumia utakuwa na thamani kubwa zaidi.

Haya yakiwa mabadiliko mamkubwa katika mtandao huo wenye watumiaji zaidi ya bilioni mbili duniani kote,itaongeza mapato kutoka kwenye matangazo.

Licha ya kuwa ,Facebook imekuwa katika shinikizo kubwa la kukabiliana na watu ambao wamekuwa wanapenda mtandao huo kupita kiasi ambacho wanaweza kuatharika na afya ya akili.