Alexis Sanchez ajiandaa kuondoka, Arsenal yamlenga mchezaji wa Brazil

Alexis Sanchez ajiandaa kuondoka, Arsenal yamlenga mchezaji wa Brazil Haki miliki ya picha EPA
Image caption Alexis Sanchez ajiandaa kuondoka, Arsenal yamlenga mchezaji wa Brazil

Mshambualiaji wa Arsenal Alexis Sanchez ataondoka katika klabu hiyo mwezi huu iwapo ombi la kuvutia litawasilishwa huku mchezaji anayechukua mahala pake akipatikana.

Inaeleweka kwamba uongozi wa Arsenal umekubali kwa wiki kadhaa kwamba Sanchez huenda akaondoka baada ya kuhudumu katika klabu hiyo kwa takriban miaka mitatu na nusu.

Hatahivyo Arsenal haiko tayari kumuuza mchezaji huyo bila kupata mchezaji mwengine atakayechukua mahala pake na kwamba wanalenga kumnunua mshambuliaji wa Bordeaux mwenye umri wa miaka 20 raia wa Brazil Malcom.

Manchester City inalenga kumsajili Sanchez mwenye umri wa miaka 29.

Mazungumzo yamefanywa kati ya vilabu hivyo viwili lakini hakuna makubaliano kuhusu malipo ya uhamisho huo.

Arsenal wamedaiwa kutaka dau la £35m, huku viongozi wa ligi ManCity wakitoa pendekezo la kumsajili kwa £20m.

Duru zimearifu kwamba makubaliano ya uhamisho wa kati ya £25m na £30m yameafikiwa.

Pia imeripotiwa kwamba Manchester United watashindana na City katika kumsajili mchezaji huyo na tayari wamewasilisha ombi lao.

Iwapo hakutakuwa na makubaliano, Sanchez atalazimika kuondoka katika klabu hiyo wakati kandarasi yake itakapokamilika mwisho wa msimu huu hatua ambayo Arsenal inaipinga kwa kuwa huenda wasipate fedha zozote kutoka kwa mchezaji huyo.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii