Marekani kuiwekea Iran vikwazo vipya

Rais Trump na mwenzake wa Iran Hassan Rouhani
Image caption Rais Trump na mwenzake wa Iran Hassan Rouhani

Waziri wa fedha nchini Marekani Steve Mnuchin amesema kuwa anatarajia rais Donald Trump kuiwekea vikwazo vipya Iran.

Habari hiyo inajari wakati ambapo Trump anakabiliwa na tarehe ya mwisho kuamua iwapo ataiondolea Iran vikwazo vingine vilivyoondolewa chini ya makubaliano ya kinyuklia ya 2015.

Mapema, mataifa ya Ulaya yenye uwezo mkubwa yalimtaka Trump kuafikia makubaliano hayo yakisema ni muhimu kwa usalama wa kimataifa.

Bwana Trump amekosoa mpango huo ambao ulipelekea Iran kuondolewa vikwazo baada ya kukubali kupunguza mpango wake wa kupunguza uzalishaji wa mafuta ya nguvu za kinyuklia.

Bwana Mnuchin aliambia maripota kwamba alitarajia vikwazo vipya dhidi ya Iran kutangazwa -ambavyo kulingana na ripoti za awali vinalenga watu binafsi na biashara nchini Iran.

''Tunaendelea kuvitathmini na nafikiri tutarajie kwamba kuna vikwazo zaidi''.

Rais uyo wa Marekani anasema kuwa anataka kuufanyia marekebisho muswada huo ama kujiondoa kabisa.

Mada zinazohusiana