Everton yathibitisha kuanza mazungumzo ya kumsajili Theo Walcott

Allardyce anataka kuimarisha safu yake ya mashambulizi na akasema kuwa Walcott mwenye umri wa miaka 28 atakuwa kiungo muhimu. Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Allardyce anataka kuimarisha safu yake ya mashambulizi na akasema kuwa Walcott mwenye umri wa miaka 28 atakuwa kiungo muhimu.

Mkufunzi wa Everton Sam Allardyce anasema kuwa klabu hiyo imeanza mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Theo Walcott kwa mkataba wa kudumu.

Allardyce anataka kuimarisha safu yake ya mashambulizi na akasema kuwa Walcott mwenye umri wa miaka 28 atakuwa kiungo muhimu.

''Hatujakubaliana lakini mazungumzo yanaendelea na tuna matumaini ya kumuajiri kwa mkataba wa kudumu'', alisema Allardyce, 63.

"Sijipatii matumaini nisije nikashangazwa. Nitafurahi sana iwapo mtu yeyeote hata iwapo sio Walcott atatia saini kanadarasi.

Allardyce, ambaye tayari amemsajili mshambuliaji Cenk Tosun kutoka Besitkas kwa kitita cha £27m mwezi Januari, amesifu kasi ya Walcott, uzoefu na uwezo wake wa kupiga krosi nzuri kuwa mchango atakaoleta katika klabu yake.

Mada zinazohusiana