Makanisa yaliyochongwa kwenye miamba Ethiopia

Makanisa yaliyochongwa kwenye miamba Ethiopia

Eneo la Lalibela kaskazini mwa Ethiopia kuna makanisa ya kale na ya kuvutia ambayo yalijengwa mwishoni mwa karne ya 12.

Makanisa hayo yaliagizwa na mfalme Lalibela ambaye alitaka kujenga Yerusalemu mpya kwa wasomi wake.

Wanahistoria wengi waliamini kwamba sanaa ya kuchonga makanisa ilikwisha zaidi ya miaka 500 iliyopita.

Lakini hata leo, uvumbuzi mpya wa makanisa hayo unaendelea na mengine mapya yanajengwa.