Wakili wa Trump adaiwa kumlipa mwigizaji wa filamu za ngono ili kunyamaza

Wakili wa rais Donald Trump Michael Cohen
Image caption Wakili wa rais Donald Trump Michael Cohen

Taarifa kwenye vyombo vya habari nchini Marekani zinadai kwamba wakili wa rais Trump alimlipa mwigizaji wa filamu za ngono zaidi ya dola laki moja, kama njia ya kumshawishi asiseme lolote kuhusu mikutano anayodaiwa kushiriki na rais Trump.

Malipo hayo yalitolewa mwezi mmoja kabla ya uchaguzi wa urais, katika wakati muhimu kwenye kampeni ya rais Trump, wakati akipuuza madai kwamba aliwadhalilisha wanawake.

Gazeti la The Wall Street Journal linasema kwamba wakili huyo, kwa jina, Michael Cohen, alilipa pesa hizo baada ya Stormy Daniels, kutishia kufichua siri zake hadharani.

Gazeti la New York Times zinasema bwana Cohen alikanusha madai ya kukutana na Bi Stormy, japo hakutaja malipo yoyote.

Mada zinazohusiana