Washukiwa 40 wa mauaji kufuatia mgogoro wa ardhi wakamatwa na polisi Tanzania

Ramani ya Tanzania
Image caption Ramani ya Tanzania

Takriban watu 40 wamekamatwa na maafisa wa polisi nchini Tanzania kufuatia mauaji ya watu wawili waliouawa kutokana na mgogoro wa ardhi wa zaidi ya muongo mmoja kaskazini mwa taifa hilo.

Mgogoro huo unashirikisha takriban hekari 4,000 za ardhi za kilimo karibu na mbuga ya kitaifa ya wanayama pori ya Serengeti.

Wawili hao waliuawa kwa kukatwakatwa mapanga siku ya Ijumaa wakati walipokuwa katika na kijiji chao cha Remng'oroni .

Washambuliaji hao ambao maafisa wa polisi wanasema walibeba mishale baadaye walitorokea katika nyumba zao katika kijiji jirani.

Mada zinazohusiana