Daktari wa White House asema Trump ana afya nzuri baada ya uchunguzi

Donald Trump shakes hands with Dr Ronny Jackson after his annual physical exam at Walter Reed National Military Medical Center in Bethesda, Maryland, 12 January 2018 Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bw. Trump akimsalimia Dr. Jackson baada ya uchunguzi

Donald Trump yuko katika hali nzuri kiafya, daktari wake wa White House ametangaza baada ya Trump kufanyiwa uchunguzi wa kiafya kwa kwanza tangu achaguliwe kuw rais.

Ronny Jackson alisema kuwa uchunguzi wa saa tatu uliofanywa siku ya Ijumaa kwa Trump mwenye umri wa miaka 71 na uliofanywa na madaktari wa kijeshi ulikuwa wa mafanikio.

Aliahidi kutoa taarifa zaidi siku ya Jumanne.

Hakuna uchunguzi wa kiakili ulipangwakufanywa lakini kitabu kimoja cha hivi majuzi kilitilia shaka hali ya kiakili ya Rais Trump.

Kulingana na Michael Wolf, mwandishi wa kitabu cha Fire and Fury: Inside the Trump White House, ni kuwa wafanyakazi wote wa White house wanamuona Trump kama mtoto.

Trump alijibu kwa kusema kuwa kitabu cha Wolff kina uwongio mwingi huku waziri wa mashauri ya nchi za kigeni Rex Tillerson akitupilia mbali madai kuwa hali ya kiakili ya rais ilikuwa haifeli

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Dr Jackson akitoa ishara baada ya uchunguzi

Mada zinazohusiana