Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu afanya ziara India

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu afanya ziara India Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu afanya ziara India

Waziri mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu, amewasili India katika ziara inayolenga kuimarisha uhusiano wa kibiashara.

Picha zilionyesha Bw. Natenyahu akiwasili India na kumpa pambaja la mwaka mwenyeji wake Narendra Modi.

Tangu Bw. Modi alipofanya ziara ya kihistoria Israeli mwaka jana, kumekuwa na mjadala kuhusu uhusiano wa karibu baina ya viongozi hao wawili.

Kwa hakika, kuna ishara ya nguvu mpya katika uhusiano wa kibiashara baina ya India na Israel

Bwana Natenyahu anaandamana na wakuu wa kibiashara kutoka Israeli, na amezungumzia mikataba mingi itakayowekwa saini katika kipindi cha siku chache zijazo, hususan katika sekta za kawi na kilimo.

India, inayotumia pesa nyingi katika sekta ya ulinzi, inataka uwekezaji zaidi ili kupata silaha za kisasa.