Kiongozi wa UKIP amtema mpenzi aliyesema watu weusi wana sura mbaya

Henry Bolton and Jo Marney Haki miliki ya picha Getty Images / @Jo_Marney
Image caption Henry Bolton na Jo Marney

Kiongozi wa chama cha UKIP nchini Uingereza Henry Bolton anasema kuwa amesitisha uhusiano na mpenzi wake baada ya yeye kuripotiwa kutoa maoni ya ubaguzi wa rangi kumhusu Meghan Markle.

Alisema kuwa mapenzi yao hayataendelea akiwa na wajibu kama kiongozi wa chama lakini hana nia ya kujiuzulu.

Jo Marney alikuwa ametuma ujumbe wa simu kuwa watu weusi wana sura mbaya na mpenzi wake Prince Harry ataichafua familia ya kifalme.

Bw Bolton alisema kuwa ilikuwa kinyume na katiba ya chama cha UKIP kuonyesha fikra zozote za ubaguzi wa rangi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kiongozi wa UKIP Henry Bolton

Mwanajeshi huyo wa zamani alichukua usukani wa chama cha UKIP kama kiongozi mwezi Septemba, na kuwa kiongozi wa nne katika kipindi cha miaka 18.

Bw Bolton 54, alisema kuwa mwanamitindo huyo wa miaka miaka 25 alitimuliwa chamani mara moja baada ya chama kugundua kuhusu maoni yake.

Ujumbe huo ulitumwa wiki tatu baada ya wapenzi hao wawili kuanza uhusiano wao.

Mada zinazohusiana