Lowassa: Magufuli aliniomba nirudi CCM

Lowassa na Magufuli walikutana Ikulu kwa mara ya kwanza baada ya uchaguzi wa 2015 Haki miliki ya picha IKULU
Image caption Lowassa na Magufuli walikutana Ikulu kwa mara ya kwanza baada ya uchaguzi wa 2015

Mjumbe wa kamati kuu ya chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, CHADEMA, Edward Lowassa amefichua kuwa Rais John Magufuli alimuomba arejee chama tawala cha CCM wakati wa mazungumzo yao juma lililopita.

Katika taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari na Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, Lowassa ameeleza: "Ujumbe wa Rais Magufuli ulikuwa kunishawishi kutaka nirejee CCM, suala ambalo sikukubaliana nalo na nilimueleza Rais ya kwamba uamuzi wangu wa kukihama chama hicho na kujiunga na CHADEMA haukuwa wa kubahatisha".

Wiki iliopita, kiongozi huyo wa upinzani nchini Tanzania, ambaye pia ni Waziri mkuu wa zamani, alikutana na Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli Ikulu na kumsifu sana kwa kazi anayoifanya.

Ni hatua ambayo iliwashangaza wengi kwani si kawaida kwa kiongozi huyo kumsifu Rais Magufuli kwani kwa muda amekuwa akikosoa utawala wake.

Bw Lowassa aliwania urais kupitia chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015 lakini akashindwa na Dkt Magufuli aliyewania kupitia Chama cha Mapinduzi.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii