Mwanamume ashtakiwa kufanya tendo la ngono na mbuzi Kenya

Mbuzi Haki miliki ya picha AFP

Mwanamume mmoja katika jimbo la Machakos nchini Kenya ameshtakiwa na kosa la kufanya tendo la ngono na mbuzi wawili.

Inadaiwa kuwa mwanamme huyo aliwaua mbuzi hao wawili baada ya tendo hilo lililowaacha wanakijiji na mshangao mkubwa.

Akifikishwa mbele ya mahakama mjini Kangundo,mashariki mwa mji mkuu wa Nairobi.

Mwanamme huyo mwenye umri wa miaka 35 alishtakiwa kosa la kuwatendea ukatili mifugo hao kwa kuwaua baada ya kitendo hicho cha kustaajabisha.

Upande wa mashtaka uliwasilisha mizoga ya mbuzi hao wawili kama ushahidi mbele ya mahakama.

Mshtakiwa kwa upande wake aliilezea mahakama kuwa alipigwa na kuumizwa vibaya na maafisa wa polisi waliomkamata.

Jaji anayesikiliza kesi hiyo aliamuru mshtakiwa huyo huyo apelekwe hospitalini kwa matibabu na kumwachilia kwa dhamana ya dola 1,000 za Marekani.

Kesi hiyo itasikilizwa tena tarehe 29 mwezi Januari mwakani.

Haki miliki ya picha HISANI

Sheria ya Kenya inatoa adhabu ya miaka 14 gerezani kwa mtu atakayepatikana na kosa la kujamiiana na mnyama.

Hata hivyo visa kama hivi vimekuwa vikiripotiwa mara kwa mara nchini Kenya.

Mwezi Machi mwaka jana, mwanamme mmoja alifungwa jela miezi 15 kwa kufanya kitendo kisicho cha kawaida na kuku akidai alikuwa mwoga sana kiasi cha kuogopa kuwachumbia wanawake.

Mada zinazohusiana