Ujumbe unaotolewa na rangi ya gari barabarani

Two people in a soft top Haki miliki ya picha Getty Images

Magari huwa ya rangi aina nyingi, lakini umewahi kujiuliza ni mambo gani mtu huzingatia kabla ya kununua gari la rangi fulani au akibadilisha rangi ya gari lake?

Rangi ya gari huwa inatuma ujumbe fulani, ingawa mmiliki wa gari huenda asifahamu hili.

Siku hizi, magari ya rangi nyeusi yamekuwa ndiyo maarufu zaidi. Utafiti nchini Uingereza unaonesha magari ya rangi nyeusi yalikuwa ndiyo mengi huko mwaka 2017, yakifuatwa na magari ya rangi ya kijivu na magari ya rangi nyeupe yakawa ya tatu.

Mwanasaikolojia anayeangazia masuala ya rangi Angela Wright anasema rangi nyeusi huonesha mmiliki wa gari hilo ni mtu anayetaka kujihisi salama na kuwa salama.

Haki miliki ya picha Getty Images

Aliambia BBC: "Si ajabu kwamba wengi wameanza kutumia sana rangi nyeusi.

"Ni rangi ambayo watu wanaweza kujificha nyuma yake na ni kama blanketi au kinga kwa watu ambao hawana ujasiri wa kukumbatia rangi nyingine."

Nyeupe au Kijivu

Haki miliki ya picha Getty Images

Baada ya rangi nyeusi, magari ya kijivu yalifuata kwa kuwa mengi Uingereza (19.7%).

Angela anasema rangi hii inaonesha mtu wa kushikilia maadili, anayependa kujificha, na pia hali mbaya ya hewa.

Anasema kuwepo kwa rangi hiyo wakati mwingine huwafanya watu kufadhaika.

"Ukipaka gari lako rangi ya kijivu, huenda unajaribu kuhifadhi pesa."

Magari ya rangi nyeupe o(19%) yamo nafasi ya tatu na Angela anasema hii ni ishara ya kutoegemea upande wowote, na kutaka pia kuwa salama.

Buluu na nyekundu

Haki miliki ya picha Getty Images

Rangi ya buluu (16%) mara nyingi hupendwa na watu kwa sababu huashiria utulivu, huonesha utaratibu na hutuliza fikira anasema Angela.

"Ukinunua gari la buluu, basi pengine una kitu ambacho unatamani sana unachoamini kitaongeza maana maishani na pengine wewe ni dereva mmakinifu sana," anaongeza.

Rangi nyekundu ni ya sita kwa umaarufu (9.9%), na Angela anasema wengi watakuwa ni wanaume.

Rangi hii huashiria nguvu na mamlaka na huongeza shinikizo kwenye damu ukiiona, na husisimua watu pia.

Rangi ya njano

Haki miliki ya picha Getty Images

Ni 0.4% pekee ya magari Uingereza ni ya rangi ya manjano.

Angela anasema: "Hii ina maana kwamba wewe ni mmoja wa watu wenye matumaini makubwa sana maishani na pengine wewe ni mpenda urafiki."

Wauzaji magari wa Arnold Clark wanasema magari haya huwa ndiyo salama zaidi, pengine kwa sababu huonekana vyema barabarani.

Wanasema pia magari ya rangi nyeusi ya uwezekano 47% wa kuhusika kwenye ajali.

Mada zinazohusiana