Barua kutoka Afrika: Jamii za makundi ya WhatsApp barani Afrika

Wanawake wawili wakipiga selfie kabla ya fesheni ya swahili mjini Dar es Salaam, Tanzania tarehe 4 Disemba 2015 Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanawake wawili wakipiga selfie kabla ya fesheni ya swahili mjini Dar es Salaam, Tanzania tarehe 4 Disemba 2015

Katika msururu wa barua kutoka kwa waandishi wa bara Afrika , Joseph Warungu anatazama makundi ya mtandao wa WhatsApp ili kujua wasimamizi wa makundi hayo ni akina nani.

Nimepandishwa ngazi kuwa msimamizi wa kundi moja la WhatsApp kwa lengo la kutafuta usaidizi wa miradi ya maendeleo katika kijiji chetu nchini Kenya.

Kwa kubofya tu naweza kumuondoa mwanachama yoyote katika kundi hilo.

Hivyobasi nimekuwa silali muda mwingi nikichunguza yanayoendelea katika kundi hilo nikingojea ni nani atakayekiuka sheria zinazoendesha kundi hilo.

Sikujua kwamba uongozi huwa tamu hivi. Kwamba naweza kumchukulia hatua mtu yeyote atakayesambaza picha nyingi na video za ''mbuzi akicheza densi na paka''?

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Watu wakidurusu mitandao yao ya kijamii kwa kutumia simu aina ya smartphone

Mtandao wa WhatsApp umebadilisha vile tunavyowasiliana. Pia ni chanzo cha habari , habari nzuri, mbaya ama hata bandia.

Mtandao wa WhatsApp pia umewahi kuvunja uhusiano wa kimapenzi na ule wa kirafiki.

Ni kifaa kinachoweza kuwavutia watu wengi kinachokuwezesha kupata aina yoyote ya habari kutoka kokote.

Katika kundi moja la wanahabari ambalo mimi mwenyewe ni mwanachama, inakuchukua sekunde chache kupata nambari za simu ya karibia Mkenya yeyote.

Katika kundi jingine, kuna harakati za kuanzisha biashara ambayo inafadhiliwa na wanachama wa kundi hilo.

Kuna majirani na jamii ambazo ziko katika makundi ya WhatsApp.

Kundi moja kama hilo mjini Nairobi linaendeshwa kupitia sheria kali.

Hakuna siasa, hakuna maswala ya kidini, hakuna utani.

'Kuokoa maisha kupitia WhatsApp'

Hivi majuzi, rafiki yangu Mkenya aliyetaka kusafiri kuelekea India ili kufanyiwa matibabu ya dharura alifanikiwa kuchangisha takriban $20,000 (£14,500) chini ya siku mbili kupitia kampeni ya mtandao wa WhatsApp.

Rafiki yangu mmoja kutoka Ghana aliniambia yuko katika kundi la watu wenye ushawishi mkubwa ambapo mmmoja wao alichapisha barua ndefu kwamba atajiua.

Wanachama wa kundi hilo mara moja walitafuta njia za kumsaidia kijana huyo.


Joseph Warungu:

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanawake wawili wakipiga selfie kabla ya fesheni ya swahili mjini Dar es Salaam, Tanzania tarehe 4 Disemba 2015

"Alichanganyikiwa na nambari za simu katika mtandao wake na ujumbe aliotarajia kuutuma kwa mkewe uliishia kwa mamake wa kambo.


Lakini kwa bahati mbaya ,wakati usaidizi ulipokuwa ukijaribu kumfikia alikuwa tayari amejiua.

Kundi hilo lilibadilika na kuanza kumuenzi mtu huyo.

Thamani ya WhatsApp inajulikana sana.

Kutokana na uzoefu wangu mimi mwenyewe nimekuwa nikichunguza wasimamizi sita wa WhatsApp huku nikitaka kumuiga mmoja wao.

1: Madikteta wa WhatsApp

Hawa ni wazimamizi wa makundi ya WhatsApp wenye njaa ya kuwa na mamlaka.

Hakuna mtu aliyewachagua lakini kila mtu anawaogopa.

Wanaendesha kundi hilo kama chombo chao cha kibinafsi.

Jaribio lolote la kuwasilisha maono ambayo hayaungi mkono tabia yao hukabiliwa vikali.

Hawataki kumuacha mtu yeyote kuondoka katika kundi hilo.

Iwapo utajaribu kuondoka unaregeshwa mara moja.

Mimi hukiita ''kifungo cha nyumbani''.

Rafiki yangu mmoja wa Afrika Magharibi aliniambia vile dikteta mmoja wa kundi la WhatsApp alivyoondolewa katika kundi hilo baada ya kupoteza simu yake.

Alimbembeleza kaimu msimamizi wa kundi hilo kumrudisha akiwa na nambari mpya ya simu.

Na mara tu alipochukua mamlaka yake tena alimfurusha kaimu msimamizi wa kundi hilo.

Afisa mmoja wa jeshi ambaye ni mwanachama wa kundi hilo ambaye ametulia aliingilia kati ili kaimu huyo arudishwe.

2: Wanaozungumza peke yao

Hawa ni wasimamizi wanaopenda sauti zao.

Hupatikana katika makundi madogo madogo yalio na wanachama wachache.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mtu amesimama katika dula la kuuza simu tarehe 1 mwezi Oktoba 2012 mjini Nairobi Kenya

Ninatoka katika kundi moja kama hilo ambalo liliundwa kwa sababu ya mazoezi lakini baadaye wanachama wengi waliondoka.

Lakini msimamizi wa kundi hilo huonekana akisema: Habari ya asubuhi watu wangu wenye furaha na bashasha, ningependa kuwatakia siku njema!

Lakini hakuna jibu kwa sababu hakuna mtu katika kundi hilo.

Kile unachoona ni msimamizi akitoa sauti yake mara kwa mara .

3: Mafia

Hawa sio wasimamizi wa kweli. lakini ndio walio na nguvu nyuma ya msimamizi.

Wanavunja uhusiano katika kundi hilo na wanaamua ni nani anayefaa kusalia na ni nani hafai.

Wakati maslahi yao yanapokuwa hatarini wanajitokeza na kuchukua uongozi huku wakionyesha muongozo wa kundi hilo kwa kifua.

4: Viongozi waasi

Hawa ni wasimamizi wa WhatsApp ambao husahau wao ndio viongozi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Watu wanatembea wakizungumza kwa simu tarehe mosi Oktoba 2012 mjini Nairobi Kenya

Wao ndio wa kwanza kuchapisha picha za fedheha , kuzua uhasama miongoni mwa wanachama walionyamaza na kuwa suluhu.

Hufanya uanaharakati hadi Ikulu bila kusahau mabango yao.

5: Wanaopenda kufurahisha watu

Hawa ni kinyume na wasimamizi madikteta. Wanaukumbatia ulimwengu.

Yeye huwa na msimamo wa kadri ,ikimaanisha kwamba kundi hilo huwa na kelele, hakuna msimamizi na sheria hazifuatwi.

Matokeo yake ni kwamba mamlaka yao huchukuliwa na watu wengi wanaotaka kusimamia kundi hilo.

6: Wakosoaji wakubwa wa maandishi yalio na makosa

Hawa ni kama walimu. Hufurahia maandishi yalio na makosa ya herufi.

Huwashika sikio wanaofanya makosa kama hayo na kuwarudisha shule.

Bahati yako ni mbaya iwapo huwezi kusahihisha maandishi katika simu yako aina ya smartphone.

Ni wapelelezi wa maswala ya maadili na ujumbe wowote unaotishia watu wazima hutolewa kwa haraka.

Rafiki yangu mmoja ambaye alifunga ndoa hivi majuzi kwa bahati mbaya alituma ujumbe kuhusu mipango yake kwa mkewe baada ya chakula chao cha jioni kusherehekea kuzaliwa kwake.

Alichanganyikiwa na nambari za simu na badala yake ujumbe huo ukamfikia mamake wa kambo.

Makosa hayo ni sherehe kwa wakosoaji wakubwa wa maandishi.

Maono yangu

Kuna vitu ambavyo siwezi kukubali kama msimamizi mpya wa kundi la WhatsApp

Kwa kuamua kuwa msimamizi , wanachama wangu wamekubali nichukue mamlaka juu yao.

Na iwapo watatumia sauti zao kuwasiliana mimi bado nina malaka ya kuwanyamazisha.

Na kwa sababu serikali ya Kenya ina uwezo wa kuwachukualia hatua kali wasimamizi kwa chochote kitakachosambazwa katika makundi hayo , nitahakikisha kuwa nimejua ni nani aliyechapisha picha ya panya anayeimba: ''Uwezo wa wasimamizi wa makundi ya WhatsApp unakiuka katiba''!

Mada zinazohusiana

Kuhusu BBC