Nilitaka mtoto tu, nikaangukia mahabani

Ulaya
Image caption Tangazo la kumsaka mwenza na vigezo vyake

Miezi kumi iliyopita, kwenye tarehe kama thelathini hivi Jessica alikuwa na mshawasha wa kupata ujauzito.

Mahusiano yake ya awali mara kadhaa hayakuzaa matunda hivyo basi akaamua kuja kujaribu njia mpya sana, akaweka tangazo kwenye mtandao wa kijamii.

Na matokeo yalikuwa mazuri mno kuliko alivyotarajia.

Tangazo hilo lilisomeka hivi; njia salama mbadala ya ujauzito, anasema Jessica nina umri wa miaka 30 na nimeshabwaga manyanga ya kumpata mume wa ndoto zangu na hata hao wasostahili, Ninachotaka ni mtoto tu.

Tangazo hili liliwekwa katika tovuti ya Craigslist, tovuti maarufu kwa kuuza bidhaa kuu kuu.

Akaeleza muonekano wa baba mtoto wake anavyopaswa kuwa, awe na zaidi ya urefu wa futi 5 inchi 9 awe na umri chini ya miaka 40 na awe tayari kwenda kufanya vipimo vya magonjwa ya zinaa, kama haitoshi ajue kwamba analo jukumu la kuwa na siku za kukutana kimwili kwa siku kadhaa mfululizo.

Tambua tu kuwa alilituma tangazo hilo wakati akiwa ndani ya basi njiani kurejea nyumbani katika vitongoji katikati mwa London, na wakati anafika mwisho wa safari yake mtaa wa Oxford alikuwa na mrejesho wa hao mababa watarajiwa wakionehsa ukubalifu wao.

Anaeleza haja ya moyo wake kuwa, alifanya maamuzi ya kujitoa muhanga kujiridhisha kimahaba mradi watoto wake wawe na wazazi wawili wanaowapenda na kuwajali na kwa hatua hiyo haoni sababu ya kuutaka radhi umma kwa njia aliyotumia.

Basi akaamua kufanya miadi na miongoni mwao ambao walikuwa mafundi wa kujinadi kwake .

Image caption uhusiano una safari

Anatazama nyuma , kuhusiana na historia kuwa wazee wao hawakutumia miaka na miaka wakiangalia masanduku ya nguo, lah hasha, bali uanzishwaji wa familia lilikuwa ni suala la kipaumbele kwao, anasema marafiki zake walio wengi waliingia kwenye uhusiano madhubuti baada ya kuzama mahabani ingawa baadaye waliweza kuachana wakiwa katika wingu zito la hasira.

Lakini mwaka mmoja baadaye, Jesicca alikuwa katika uhusiano maridhawa na bwana mmoja akiitwa David Scott. Kama alivyo yeye, naye alikuwa anataka watoto.

Lakini hakuwa na haraka, lakini miezi sita ya majaribio haikuzaa matunda, vipimo vilionesha kuwa Jessica alikuwa sawa isipokuwa David aliyekuwa na matatizo ya uzazi, taarifa ambayo hakuipokea vyema .Kwani alikata tamaa na mwishowe waliachana.

Kwa mara ingine, kijana mmoja aliniandikia na kusema anatamani mno kupata watoto baada ya mpenzi waliyeachana kuviza mimba, Jessica akajiona yu hatarini.

Kisha tena akapokea barua pepe kutoka kwa Ross.

Wakakubaliana kukutana kwa kinywaji jioni moja. Jessica na Ross baada ya mazungumzo ya kina wakapiga muhuri wa mwanzo wa uhusiano wao mpya kwa busu mwanana , Jessica akashuhudia kuwa alijisikia vizuri mno kuwa karibu na mpenzi wake mpya.

Image caption Kiu ya kupata watoto yachipuza

Lakini wiki kadhaa baadaye akapokea majibu ya vipimo vyake kuwa ameshika ujauzito karibu kabisa na kuingia kwenye siku zake , anasema kuwa alijikuta amepata ujauzito wiki sita tu tangu tangazo lile, kilikuwa kitu cha kumshangaza mno, anasema hakutegemea kabisa.

Jessica anasema halijutii tangazo lile, na huwezi kujikalia tu ukitegemea kila kitu kitakufuata miguuni pako, lah hasha.

Jaribu, jaribu tena na tena utafanikiwa katika hitaji na haja ya moyo wako.

Mada zinazohusiana