Kunguru alazimu ndege ya wanajeshi wa AMISOM kutua Burundi

Picha ya Kunguru Haki miliki ya picha AFP
Image caption Picha ya Kunguru

Kunguru mmoja amelazimu ndege iliokuwa imewabeba wanajeshi wa Amisom kutoka Burundi kutua kwa ghafla katika uwanja wa ndege wa Bujumbura nchini Burundi.

Ndege hiyo inadaiwa kumgonga kunguru huyo angani wakati ilipokuwa ikipaa , kabla ya rubani kuamua kutoendelea na safari ya kuelekea Somalia ambapo wanajeshi hao wanahudumu kulingana na vyanzo vya habari na wizara ya ulinzi katika uwanja huo.

Ndege hiyo ilisalia hewani kwa takriban saa moja kabla ya kutua.

Huwezi kusikiliza tena
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ametangaza kuwa serikali yake inajiandaa Kuishtaki EU

Wanajeshi wa Burundi ni miongoni mwa wananjeshi wa Umoja wa Afrika wanaokabiliana na wapiganaji wa Al-Shabab nchini Somalia.

Image caption Wanajeshi wa AU nchini Somalia

Afisa mkuu wa uwanja wa ndege wa Burundi Emmanuel Habimana amethibitisha kuwa ndege hiyo iligonga kunguru huyo mepama alfajiri.

Hatahivyo kulingana na afisa huyo hakukuwepo na tatizo lolote la kiufundi na ndege hiyo iliondoka tena.