Korea Kusini yasema iko macho kwa kaskazini

Viongozi wa Korea kaskazini na kusini walipokutana Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Viongozi wa Korea kaskazini na kusini walipokutana

Korea kusini imesema itashughulika na Korea kaskazini kwa kile alichokiita '' Macho ya wazi'' baada ya kukamilika mpango wa kuweka timu moja ya pamoja katika michezo ya majira ya baridi ya Olympics inayofanyika mwezi ujao.

Akizungumza na BBC Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Korea kusini Kang Kyung-wha amesema licha ya makubaliano yaliyopo, dhumuni kubwa linabaki kuwekwa vikwanzo kushughulika na vitisho vya nyuklia.

Amesema mkutano uliojumuisha nchi 20, ambao umefanyika katika mji wa Vancouver ulikuwa ukihusu jinsi bora ya kuweka vikwazo hivyo. Lakini pia amezingatia mahitaji ya kibinadamu kwa watu wa Korea kaskazini.

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Korea Kusini Kyang Kyung-what ameupongeza ushirikiano huo kati ya nchi yake na kaskazini.

Amesema pia anataka kuona misaada ya kibinadamu ikipelekwa Korea kaskazini.

Katika hatua nyingine, Waziri wa Mambo ya nchi za nje wa Marekani Rex Tillerson, amesema nchi yake na washirika wao ikiwemo China, haijawahi wakaunganika pamoja kama sasa dhidi ya kitisho cha nyuklia kilichowekwa na Korea kaskazini.

Mada zinazohusiana