Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 20.01.2018

Alexi Sanchez Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Alexi Sanchez

Kocha wa zamani wa Barcelona Luis Enrique ameorodheshwa miongoni mwa makocha wanaotarajiwa kumrithi Mkufunzi wa Chelsea Anonio Conte mwishoni mwa msimu huu huku aliyekuwa beki wa Cheslea Juliano Belletti akiwa mkurugenzi wa kandanda. (Star)

Na mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola anasakwa na klabu ya Paris St-Germain. (Mirror)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kiungo wa kati wa Brazil Malcom

Tottenham inatarajiwa kuishinda Arsenal katika kumsajili mchezaji wa Brazil na Bordeaux mwenye umri wa miaka 20 Malcom. (Telegraph)

Huenda mkataba haujaafikiwa lakini Mkufunzi wa Manchester Pep Guardiola ameipongeza Manchester United kwa kumsajili mshambuliaji wa Arsenal na Chile Alexis Sanchez, 29. (Talksport)

Image caption Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola

Manchester City ilijiondoa katika harakati za kutaka kumsajili Alexis Sanchez kutoka Arsenal huku wakihofia kwamba hatua hiyo itaathiri vibaya udhabiti wa kifedha wa klabu hiyo.(Times - subscription required)

Kiungo wa kati wa Armenia Henrikh Mkhitaryan aliwaaga wachezaji wenzake wa Manchester United baada ya fursa ya mwisho ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28-ya kufanya mazoezi na wenzake kabla ya uhamisho wake wa kuelekea Arsenal. (Mail)

Image caption Mourinho na winga wa man United Henrikh Mkhitaryan

Alexis Sanchez huenda akaichezea Arsenal dhidi ya Crystal Palace siku ya Jumamosi baada ya kurudi katika mazoezi siku ya Ijumaa baada ya kufanya mazoezi na timu ya vijana.. (Mirror)

Lakini inadaiwa kulikuwa na maafikiano ya mkataba huo baadaye siku ya Ijumaa ambayo yalimlazimu Alexis Sanchez kuwaaga wachezaji wenzake wa Arsenal na kuondoka katika hoteli ya timu hiyo huku Gunners wakijiandaa kukabiliana na Crystal Palace. (Express)

Image caption Mshambuliaji wa zamani wa man United Javier Hernandez

Mkufunzi wa Newcastle Rafael Benitez amekataa kuhakiki hatma yake katika klabu ya Newcastle United huku akisubiri klabu hiyo kuwasajili wachezaji watatu au wanne katika kikosi chake wakati wa dirisha la uhamisho la mwezi Januari. (Guardian)

Liverpool walikuwa wanajiandaa kumnunua kipa wa Stoke Jack Butland kwa dau la £40m lakini wameambiwa kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 hauzwi (Express)

Image caption Kipa wa Stoke na Uingereza Jack Butland

Aliyekuwa mshambuliaji wa Manchester United Javier Hernandez hatorudi katika klabu hiyo huku Besiktas ikimnyatia kwa dau la £7.5m (8.5m euro) (Goal)

Norwich inakaribia kukamilisha usajili wa mchezaji wa klabu ya Eintracht Braunschweig's Onel Hernandez, 24. (Sun)

Everton inamtaka beki wa klabu ya Lille Adama Soumaoro, 25, lakini bado hawajawasilisha ombi la kumsajili mchezaji huyo.(Liverpool Echo)

Image caption Beki wa Ureno Bruno Alavez

Beki wa Rangers raia wa Ureno Bruno Alves, 36, anasakwa na klabu ya Itali Benevento. (Sky Italia - in Italian)

Mkufunzi wa Southampton Mauricio Pellegrino amesema kuwa klabu hiyo ilifanya kila kitu ili kujaribu kumnunua aliyekuwa mshambuliaji wa Arsenal Theo Walcott kabla ya mchezaji hyo kuelekea Everton (Southampton Echo)

Image caption Mshambuliaji wa Bournemouth Benik Afobe

Bournemouth ina fuaraha ya kumuuza mshambuliaji Benik Afobe mwezi huu lakini inataka kupata £10m walizolipa kwa Wolves kumsajili mchezaji huyo 24 miaka miwili iliopita . (Sun)

Crystal Palace imewasilisha ombi la kumsajili mshambuliaji wa Inter Milan na Itali Eder ,31, kwa dau la £9.75m . (Corriere dello Sport, via Croydon Advertiser)

Mada zinazohusiana