Kunguni: Ghana yaionya kampuni ya ndege ya British Airways

Kunguni: Ghana yaionya kampuni ya ndege ya British Airways Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kunguni: Ghana yaionya kampuni ya ndege ya British Airways

Waziri wa maswala ya angani nchini Ghana Cecelia Dapaah ameionya kampuni ya ndege ya British Airways kwamba huenda ikakabiliwa na vikwazo kufuatia ripoti ya kunguni katika baadhi ya ndege zake zinazoingia nchini humo.

Gazeti la Uingereza wiki hii liliripoti kwamba ndege moja ya kampuni hiyo iliokuwa ikielekea mjini Accra ilizuiwa katika uwanja wa Heathrow kwa saa kadhaa baada ya wadudu hao kuonekana wakitambaa katika viti vyake.

British Airways ambayo ina ukiritimba wa ndege kati ya Uingereza na Ghana imetoa taarifa ikisema kuwa kisa kama hicho sio cha kawaida ma kundi la wataalam limechukua hatua za haraka kukabiliana na tatizo hilo.

Gazeti la The Sun lilichapisha habari kuwa wahudumu wa ndani ya ndege hiyo walipigwa na butwaa walipowaona kunguni wengi tu ndani ya ndege na kulazimu kuahirishwa kwa safari yao.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kunguni

Wahudumu hao walizua taharuki walipokurupuka nje badala ya kuwaelekeza wasafiri kuingia ndani ya ndege hiyo.

Kamuni hiyo iliambia BBC kwamba Ghana ni taifa muhimu kwa kampuni hiyo.

Mada zinazohusiana