Arsenal, Chelsea na Man United zawika EPL

Wachezaji wa Arsenal wakifurahia ushindi wa mabao manne dhidi ya Crystal Palace
Image caption Wachezaji wa Arsenal wakifurahia ushindi wa mabao manne dhidi ya Crystal Palace

Arsenal iliicharaza Crystal Palace 4-1 huku Chelsea ikiifunga mdomo Brighton 4-0 katika mechi za ligi ya Uingereza siku ya Jumamosi.

The Gunners walikosa huduma za mchezaji Alexis Sanchez, ambaye anatarajiwa kujiunga na Manchester United, lakini walikuwa wakiongoza kwa bao 4-0 baada ya dakika 22.

Image caption Willian na nyota wa Chelse\ Eden Hazard

Eden Hazard alikuwa nyota wa Chelsea, baada ya kufunga mara mbili huku timu ya the Blues ikishinda mechi yao ya kwanza katika mwaka mpya wa 2018.

Manchester United ambao wako katika nafasi ya pili walipata ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya wenyeji Burnley, kufuatia bao la Anthony Martial na hivyobasi kupanda wakiwa pointi sita nyuma ya viongozi Manchester City, ambao wanakabiliana na Newcastle katika mechi ya mwisho (17:30 GMT).

Mkufunzi mpya wa Stoke Paul Lambert alianza vizuri , baada ya kuiongoza City kuondoka katika eneo la kushushwa daraja kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Huddersfield, kufuatia mabao ya Joe Allen na Mame Biram Diouf.

Image caption Mshambuliaji wa Everton Oumar Niasse

Oumar Niasse naye aliiokoa Everton dhidi ya West Brom, lakini mechi hiyo ilitawaliwa na jeraha baya lililomkabili James Mccarthy ambaye aliondolewa uwanjani kwa machela.

Penalti ya Jamie Vardy na bao la Riyad Mahrez lilisaidia Leicester City kuendeleza msururu wa matokeo mabaya wa Watford

Nayo West Ham ilitoka sare ya 1-1 na Bournemouth, baada ya bao la Ryan Fraser la dakika ya 71 kusawazishwa sekunde 69 baadaye na Javier Hernandez.

Mada zinazohusiana