Uturuki inasema wanajeshi wake wa nchi kavu wameingia Syria

Wanajeshi wa Uturuki karibu na mpaka wa Syria Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wanajeshi wa Uturuki karibu na mpaka wa Syria

Waziri mkuu wa Uturuki Binali Yildirim amesema wanajeshi wa nchi kavu wamevuka na kuingia katika ngome ya Afrin kaskazini mwa Syria inayodhibitiwa na waKurdi.

Wanamgambo wa KiKurdi, YPG wamekana taarifa hizo wakieleza kuwa shambulio la Uturuki lilizimwa.

Wanajeshi wa Uturuki wanaoungwa mkono na wapiganaji wa upinzani Syria waliingia kaskazini mwa Syria baada ya saa tano asubuhi Jumapili.

Ndicho anachokisema waziri mkuu wa Uturuki -- siku moja baada ya Uturuki kuingia katika eneo jipya katika vita vua Syria huku kukiwepo makombora makali dhidi ya maeneo yanayodhibitiwa na Wakurdi Syria.

Yildirim anasema lengo la nchi yake ni kuidhinisha eneo salam la kilomita 30 katika enoe hilo.

Haki miliki ya picha AFP

Wanamgambo wa Kikurdi wanasema wamezima shambulio la vikosi vya Uturuki baada ya makbiliano makali.

Wamekuwa mojawapo ya vikosi vyenye nguvu nchini Syria, lakini watakabiliwa na wakati mgumu kuepuka nguvu ya jeshi la Uturuki.

Wameungwa mkono na Marekani walipochangia kulitimuwa kundi la I-S, lakini inaonekana ni kama hawawezi kutegemea uungwaji mkono wa aina hiyo katika vita vya sasa.

Ni kwanini Uturuki inalenga makundi yanayoungwa mkono na Marekani?

Kundi la wanamgambo wa YPG limekuwa msaidizi mkuu katika vita dhidi ya Islamic State nchini Syria, na limeungwa mkono na Marekani.

Hatahivyo Uturuki inaamini kuwa kundi hilo linashiriikiana na kundi lililopigwa marufuku la believes the group has links to the banned Kurdistan Workers Party (PKK), na kwa miezi kadhaa imetishia kuwatimua wapiganaji wa Kikurdi kutoka Afrin na mji mwingine, Manbij, uliopo kilomita kutoka eneo hilo 100.

Haki miliki ya picha AFP

Mipango ya jeshi la Uturuki inaonekana kushika kasi kufuatia tangazo kutoka kwa Marekani kwamba itausaidia muungano wa SDF kujenga kikosi kipya cha ulinzi wa mpakani kuzuia kurudi kwa wanamgambo wa IS.

Makundi ya YPG na SDF yanakana kuwana uhusiano wowote wa kigaidi - tuhuma inayoungwa mkono na serikali ya Marekani.

Lakini rais Recep Tayyip Erdogan amekitaja kikosi hicho cha mpkani kama "jeshila kigaidi".

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii