George Weah: Mchezaji nyota alivyoibuka na kuwa rais wa Liberia

George Weah: Mchezaji nyota alivyoibuka na kuwa rais wa Liberia

Mchezaji wa zamani wa klabu za Monaco, AC Milan na Chelsea George Weah ameapishwa kuwa rais wa Liberia, na kuchukua uongozi kutoka kwa Ellen Johnson Sirleaf ambaye amestaafu.

George Weah alianza maisha yake mtaa wa mabanda lakini akang’aa sana kama mchezaji na kuwa Mwafrika wa pekee kushinda tuzo ya Ballon d’Or.

Ilikuwaje hadi mwanamume huyo anayefahamika sana kama Mfalme George Liberia akawa rais wa taifa hilo la Afrika Magharibi?