Watoto mataifa yanayoendelea wanawazidi wenzao Uingereza kwa malengo maishani

doctor
Image caption Wasichana wengi Pakistan, Bangladesh, Colombia na Indonesia wanataka kuwa madaktari

Watoto katika mataifa yanayoendelea mara nyingi wanakuwa na shauku kubwa ya kufikia malengo kuliko ya juu kuliko wavulana katika mataifa ya Uingereza, utafiti wa kimataifa unaonesha.

Wakati wavulana nchini Uingereza wakiwa na malengo ya kuwa wachezaji wa mpira wa miguu au watu maarufu katika mtandao wa YouTube, wenzao nchini Uganda na Zambia wanataka kuwa madaktari na walimu.

Matokeo ya utafiti huu yatawasilishwa kwa viongozi wakuu wa kibiashara duniani juma lijalo mjini Davos

Watafiti waliwaambia watoto wa shule ya msingi wenye umri kati ya miaka 11 katika mataifa 20 kuchora picha za kazi wanazotaka kufanya watakapokuwa watu wazima.

Wajibu wa kijinsia

Watafiti hawa walibaini kwamba kasumba ya kijinsia kwa kiwango kikubwa huanza kujikita watoto wakiwa bado na umri mdogo.

Nchini Uingereza wasichana wachache walipendelea kuwa wahandisi ama wanasayansi

Image caption Ualimu ni taalum aambayo hupendwa na watu wengi nchi mbalimbali

Lakini kazi kama uuguzi, uchezaji ngoma, na ususi zilikua miongoni mwa kazi 10 walizochagua wasichana sana.

Wavulana wao nao kazi kama urubani na umekanika zilikuwa chaguo lao la juu

Wasichana yalijikita zaidi kwenye mafanikio ya kitaaluma ambayo yangeambatana na kazi kama ualimu, matibabu ya mifugo na udaktari.

Kwa mfano wavulana walionekana kuvutiwa zaidi na tamaduni maarufu zikishabihiana na kazi kama uanamichezo, kazi katika mitandao ya kijamii au uaskari.

Kubadilisha taaluma katika jamii

Watafiti walibaini na kuelekeza kwamba ni vyema kutambulisha kazi na mifumo mbalimbali ya majukumu kwa watoto wakiwa bado katika umri mdogo

Wasichana katika shule ambazo zinaonekana kuwa na hali duni wengi wao walitaka kuwa wauza duka au wataalamu wa urembo huku wavulana katika shule bora wakitaka kuwa mameneja na wanasheria

Nje ya Uingereza michoro ilionyesha kiu na shauku ya hali ya juu licha ya mazingira magumu katika mataifa hayo.

Image caption Wavulana wengi hutaka kuwa wanasayansi na wahandisi

Uganda na Ufilipino wasichana wengi walitaka kuwa walimu.

Nchini Pakistan, Bangladesh, Colombia and Indonesia walitaka kuwa madaktari.

China kazi maarufu kwa wavulana ni uanasayansi.

Lakini kote Uingereza na kwingineko kimataifa kulikuwa na tofauti kubwa kati ya mahitaji ya soko la ajira na shauku walizo kuwa nazo vijana.

Image caption Nchini China, upishi ni kazi inayopendwa sana

Watafiti hawa wanasema kutokuwa na mpangilio bado kumeendelea kuwa kikwazo kwa wanafunzi hawa na kutoendelea kujua ni maarifa yapi wanatakiwa kuwa nayo kwa ajili ya kazi wanazozipenda.

"Ni wazi kutokana na michoro hii kuwa wanafunzi wanafika shule wakiwa na shauku kubwa ya kazi watakazopenda kufanya kutokana na mazoea ya kila siku," alisema Andreas Schleicher, msimamizi wa utafiti huo wa kielimu.

Kielelezo

Andreas aliongeza kuwa shauku ya watoto hawa inachochewa na watu wanaowajua au kuwafahamu.

Anne Lyons Rais wa Chama cha Taifa (Uingereza) cha walimu wakuu anasema inaonyesha ni kwa namna gani ilivyo ngumu kwa watoto hawa kuivunja mitazamo waliyojengewa na familia zao.

Image caption Wasichana wengi walitaka kuwa maafisa wa matibabu ya mifugo

Hizi ni kazi 10 maarufu kwa wasichana nchini Uingereza

1.Ualimu

2.Maafisa wa matibabu ya mifugo

3.Uanamichezo

4.Udaktari

5.Usanii

6.Uanamuziku

7.Ususi

8.Uanasayansi

9.Unenguaji

10.Uuguzi

Hizi ni kazi 10 maarufu kwa wavulana nchini Uingereza

1.Uanamichezo

2.Utaalamu mitandaoni

3.Polisi

4.UanaJeshi

5.Uanasayansi

6.Uhandisi

7.Udaktari

8.Ualimu

9.Maafisa wa matibabu ya mifugo

10.Umekanika

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii