Je ndio mwanzo wa kupatikana haki kwa msichana aliyebakwa Pakistan?

A candlelight vigil for Zainab in Islamabad Haki miliki ya picha Reuters

Maafisa nchini Pakistani wanasema wamemkamata mshukiwa mkuu wa kesi ya kubakwa kwa msichana wa miaka sita ambaye baadaye aliuawa, Zainab Ansari.

Afisa mkuu wa polisi katika jimbo la Punjab amemtuhumu Imran Ali, mwenye umri wa miaka 24, kwa mauaji hayo.

Akizungumza katika mkutano na waandishi habari huko Lahore, Shahbaz Sharif amesema mshukiwa huyo alikiri makosa yake na kwamba chembe chembe za vina vyake saba DNA zimelingana na sampuli zilizokusanywa kutoka eneo ambapo uhalifu huo ulitokea huko Kasur.

Haki miliki ya picha CCTV IMAGES
Image caption Kanda hiyo ya video iliomuonyesha Zainab akitembea akiongozwa na mwanamume

Hakujakuwa na tamko lolote kutoka kwa mtuhumiwa na mawakili wake.

Mauaji ya Zainab yalizusha ghadhabu kubwa kote nchini, na watu waliandamana kulalamika kuhusu kushindwa kwa polisi kukabiliana na visa hivi.

Waandamanaji wawili waliuawa katika ghasia zilizozuka.

Mwili wa Zainab ulipatikana katika jaa la taka mapema mwezi huu, siku kadhaa baadaya kupotea kwake.

Polisi huko Kasur, wanasema kumeshuhudiwa mauaji kadhaa ya aina hiyo katika miaka miwili iliyopita.

Image caption Babake Zainab, Ameen Ansari alisema, "Ni kama dunia imekwisha"

Kumekuwa na shinikizo kubwa dhidi ya polisi kuwasaka wahalifu waliohusika na mauaji ya Zainab na watoto wengine.

Familia ya Zainab inasema polisi haikuchukua hatua baada iliporipoti kuhusu kupotea kwake, na ni jamaa zao waliofanikiwa kupata kanda ya CCTV zilizoonyesha alipo onekana mwisho.

Ni kanda hiyo ya video iliomuonyesha Zainab akitembea akiongozwa na mwanamume iliyosambazwa pakubwa katika mitandao ya kijamii duniani.

Babake Zainab, Ameen Ansari, anasema baada ya kutoridhishwa awali kwa namna ya uchunguzi ulivyokuwa ukiendeshwa, sasa ana imani kesi inashughulikiwa ipasavyo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Geo News, mshukiwa anatambuliwana familia hiyo. Lakini Ansari amekana tuhuma kuwa ni jamaa yao.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii