Kuvuta sigara moja kwa siku inaongeza hatari magonjwa ya moyo na kiharusi

Man smoking Haki miliki ya picha Getty Images

Wavuta sigara wanahitaji kuacha kabisa kuvuta badala ya kupunguza uvutaji ili kuepuka hatari ya magonjwa ya moyo na kiharusi, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na jarida la utafiti wa masuala ya afya la BMJ.

Watu wanovuta sigara moja kwa siku wanauwezekano wa asilimia 50 zaidi kupata magonjwa ya moyo na wanauwezekano wa asilimia 30 wa kupatwa na kiharusi kuliko watu amabo hawajawahi kuvuta sigara,watafiti wamesema.

Wamesema inaonesha kuwa hamna kiwango salama cha uvutaji wa sigara kwa magonjwa hayo.

Lakini wataalam wamesema watu wanaopunguza uvutaji wanauwezekano mkubwa wakuacha tabia hio kabisa.

'Kuacha kabisa'

Ugonjwa wa moyo na sio saratani, ni hatari kubwa zaidi ya kifo kupitia kuvuta sigara, ikisababisha asilimia 48 ya vifo vya mapema vinavyohusiana na uvutaji sigara.

Wakati idadi ya watu wazima wanaovuta nchini Uingereza imekuwa ikishuka, idadi ya watu wanaovuta sigara moja hadi tano kila siku imeendelea kupanda,watafiti hao wamesema.

Image caption Baadhi ya wakenya wametoa maoni yao kuhusu tafiti hio ya BMJ
Image caption Baadhi ya wakenya wametoa maoni yao kuhusu tafiti hio ya BMJ

Utafiti huo umesema kuwa wanaume wanaovuta sigara moja kwa siku wanauwezekano wa asilimia 48 wa kupata ugonjwa wa moyo na wanauzekenao wa asilimia 25 wa

kupata kiharusi kuliko wale ambao hawajawahi kuvuta kabisa.

Kwa upande wa wanawake, wako katika hatari zaidi - asilimia 57 wanaweza kupata ugonjwa wa moyo na asilimia 31 kupata kiharusi.

Profesa Allan Hacksaw wa taasisi ya saratani UCL katika chuo cha College London amesema ongezeko la hatari ya magonjwa ya moyo yapo katika kipindi cha muda mrefu lakini uharibifu waweza fanyika katika kipindi cha miaka michache tu.

Lakini ameongezea kuwa habari njema ni wale watakao acha kabisa kuvuta sigara wanaweza kupunguza kwa haraka zaidi hatari ya kupata ugonjwa wa moyo.

Mada zinazohusiana