Watu 16 wafariki kutokana na homa ya Lassa Nigeria

Ugonjwa huo ambao husambazwa na panya walioambukizwa na kupitia mtu mmoja hadi mwingine.
Image caption Ugonjwa huo ambao husambazwa na panya walioambukizwa na kupitia mtu mmoja hadi mwingine.

Maafisa wa afya nchini Nigeria wanasema kuwa takriban watu kumi na sita ikiwemo wafanyikazi wa afya wamefariki kutokana na homa ya Lassa nchini humo.

Makumi ya wengine wanatibiwa ugonjwa huo ambao husambazwa na panya walioambukizwa na kupitia mtu mmoja hadi mwingine.

Kulingana na mwandishi wa BBC Is'haq Khalid mamlaka ya afya inasema kuwa zaidi ya watu sitini wameambukizwa ikiwemo wafanyikazi 10 wa afya tangu kuanza kwa mlipuko wa ugonjwa huo nchini Nigeria mapema mwezi huu.

Kituo cha kudhibiti magonjwa kimesema kuwa kinashirikiana na shirika la afya duniani na taasisi ya marekani ya kudhibiti kuenea kwa magonjwa ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo ambao umeenea katika majimbo kumi kati ya majimbo 36 ya taifa hilo.

Majimbo matatu ya Ebonyi, Ondo na Edo kusini mwa taifa hilo yameathiriwa vibaya.

Huku watu 16 wakiwa tayari wamefariki , mamlaka imewataka raia kuhakikisha kuwa kuna usafi wa kibinafsi pamoja na ule wa mazingira.

Mada zinazohusiana