Afrika Wiki hii kwa Picha: 19 - 25 Januari 2018

Mkusanyiko wa picha bora kutoka Afrika na kuhusu Waafrika wiki hii:

Liberians cheer as they stand in line to enter the inauguration off the President-elect, George Weah, at the Samuel Kanyon Doe stadium, in Monrovia, Liberia, 22 January 2018. Haki miliki ya picha EPA
Image caption Nchini Liberia, mjini Monrovia, mpiga baragumu huyu anaonekana akipiga baragumu kwa furaha wakati wa sherehe ya kumuapisha nyota wa zamani wa soka George Weah kuwa rais mpya wa nchi hiyo uwanja wa Samuel Kanyon Doe 22 Januari.
A boy drinks water from a public borehole in Chegutu, 100 km west of the capital, Harare, Zimbabwe, 22 January 2018. Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mvulana nchini Zimbabwe anywa maji kutoka kwenye mfereji katika kisima eneo la Chegutu, 100km magharibi mwa mji mkuu Harare siku ya Jumatatu.
Dead fish on the dry bed of the critically low Theewaterskloof Dam in Villiersdorp, South Africa, 23 January 2018. Haki miliki ya picha EPA
Image caption Siku iliyofuata, mzoga wa samaki unaonekana katika bwawa la Theewaterskloof lililokauka Afrika Kusini katika mkoa wa Cape Magharibi ambao umekabiliwa na ukame kwa muda mrefu.
A clergy boy sprays blessed water onto patrons of the Ethiopian Orthodox church during the Timket, an Epiphany festival, in Addis Ababa, on January 19, 2018. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa huko hakuna wasiwasi wa uhaba wa maji. Hapa, mvulana mtumishi wa kanisa anaonekana akiwanyunyizia waumini maji yaliyobarikiwa katika kanisa moja la Kiothodoksi mjini Addis Ababa. Ilikuwa ni Ijumaa wakati wa sherehe ya kubatizwa kwa Yesu katika mto Jordan ambayo hufahamika kama Timket.
Young clergy girls react during the Timket, or Epiphany festival, in Addis Ababa, on January 19, 2018. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wasichana watumishi kanisani pia wanaonekana hapa wakihudhuria ibada hiyo ya Timket...
A young boy holds a candle during the Timket, an Epiphany festival, in Addis Ababa, on January 19, 2018. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wavulana hawa pia hawakuachwa nyuma.
African migrants demonstrate against the Israeli government's policy to forcibly deport African refugees and asylum seekers from Israel to Uganda and Rwanda, outside the Rwanda embassy on January 22, 2018 in the Israeli city of Herzliya. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Siku tatu baadaye Januari 22, katika jiji la Herzliya nchini Israel, wahamiaji kutoka Afrika wanaandamana dhidi ya uamuzi wa serikali wa kuwahamisha kwa lazima maelfu ya wahamiaji wa Afrika waliofika nchini humo.
A woman hangs dyed textiles in Adjame, Abidjan, Ivory Coast, 22 January 2018. Haki miliki ya picha EPA
Image caption Siku hiyo pia, mwanamke anatungika vitambaa vilivyopakwa rangi katika mji wa Abidjan, Ivory Coast. Serikali nchini humo inapanga kutumia sekta ya nguo na mavazi kuunda nafasi zaidi za ajira.
Physically challenged Ghanaians compete in the International Federation of Skate Soccer (IFSS) tournament in Accra, Ghana 20 January 2018. Haki miliki ya picha EPA
Image caption Na raia hawa wa Ghana wanaoishi na ulemavu wanaonekana hapa wakishindana katika mashindano ya soka ya kuteleza yalitoandaliwa na Shirikisho la Kimataifa la Soka ya Kuteleza mjini Accra, Ghana.
A Togolese man with body paint in the colours of the national flag and the letter C92 referring to the return to the 1992 Constitution in Togo and for the departure of the current president, watch a protest rally by women marching against Togo"s president in the capital Lome on January 20, 2018. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mjini Lome, Togo Jumamosi, mwanamume huyu aliyepakwa rangi mwilini, rangi za bendera ya taifa hilo, anashiriki maandamano ya kushinikiza familia ya Eyadema ambayo imetawala nchi hiyo kwa miaka 50 kuondoka madarakani.
Women from different organizations hold placards and lie on the ground during a protest against Kenya"s biggest referral hospital Kenyatta National Hospital (KNH) after allegations of sexual harassment on women within the hospital"s maternity wing in Nairobi, Kenya, 23 January 2018. Haki miliki ya picha EPA
Image caption Na jijini Nairobi siku ya Jumanne, wanawake hawa wenye bango la kulalamikia tuhuma za kubakwa kwa wanawake waliojifungua watoto Hospitali ya Taifa ya Kenyatta wanaonekana wakiwa wamejilaza chini.
Graduates push a stroller and walk in a campus after the 68th graduation ceremony, where more than 14 000 students received degrees, at Makerere University in Kampala, Uganda, on January 19, 2018 Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ijumaa, wanafunzi hawa wawili walikuwa miongoni mwa wengine 14,000 waliofuzu wakati wa mahafali katika Chuo Kikuu cha Makerere, Kampala.
The Statue of King Ramses II is seen on the way to the Grand Egyptian Museum in Cairo, Egypt January 25, 2018. Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mjini Cairo, Misri siku ya Alhamisi, sanamu ya karibu miaka 3,000 ya Mfalme Ramses II nayo ilihamishwa kutoka uwanja uliopewa jina lake hadi kwenye makavazi kuihifadhi isiharibiwe na jua na mvua.

Picha kwa hisani ya AFP na Reuters

Mada zinazohusiana

Kuhusu BBC