Mwenyekiti wa maswala ya fedha wa chama cha Republican tajiri Steve Wynn, ajiuzulu

Steve Wynn ni tajiri mkubwa wa biashara ya mchezo wa kamari Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Steve Wynn ni tajiri mkubwa wa biashara ya mchezo wa kamari

Mchangishaji mkuu wa fedha za kisiasa wa chama tawala cha Republican, nchini Marekani, amejiuzulu wadhifa wake kwa sababu ya madai ya kuhusika na makosa kadhaa ya bughdha za ngono.

Steve Wynn, bilionea mmoja mmiliki wa jumba la kuchezea kamari na rafiki mkubwa wa Rais Donald Trump, ametuhumiwa kwa kuhusika katika matendo kadhaa ya bughdha za kingono, dhidi ya wafanyikazi kadhaa wa kike.

Kwa mjibu wa jarida la Wall Street, Wynn -- ambaye aliachia nafasi kama mwenyekiti wa kamati kuu ya kitaifa ya Chama cha Republican maswala ya kifedh-- wakati mmoja amewahi kumlipa mpambaji wake wa makucha mamilioni kadhaa ya dola, ili kuzima madai ya kumbughudhi kimapenzi mwanadada huyo.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Steve Wynn na mkewe wa pili, Andrea Hissom, wakati wa kuapishwa kwa Rais Trump

Amepuuzilia mbali madai hayo na kusema hayana msingi wowote.

Anasema, mkewe wa zamani ambaye wangali wakizozana baada ya kutalikiana, ndiye aliyeanzisha uzushi na uvumi huo dhidi yake.

Mada zinazohusiana