Kabul yaomboleza vifo vya watu zaidi ya 100 katika bomu la gari la kuwabebea wagonjwa

Maafisa wa usalama mjini Kabul Haki miliki ya picha EPA
Image caption Maafisa wa usalama wakilinda eneo ambapo shambulio hilo lilitokea Jumapili asubuhi

Zaidi ya watu 100 sasa wanaaminiwa kuuawa katika shambulio la bomu la kujitolea muhanga mjini Kabul Jumamosi.

Mshambuliaji aliendesha gari la kubebea wagonjwa na kupita kwenye kituo cha ukaguzi cha polisi hadi kwenye mtaa wenye umati wa watu katika wilaya yenye majengo mengi ya serikali na balozi.

Serikali ya Afghanistan imetangaza Jumapili kama siku ya maombolezi , huku mazishi ya waathiriwa na msako wa manusura kwenye hospitari vikiendelea.

Kundi la Taliban la kiislam lenye itikadi kali limetangaza kuwa lilitekeleza shambulio hilo .

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Majeruhi wakisaidia mahala pa tukio

Shambulio hili lilikuwa baya kuwahi kutokea nchini Afghanistan kwa miezi kadhaa na limefanyika wiki moja baada ya shambulio lililotokea kwenye hoteli moja mjini Kabul ambapo watu 22 waliuawa.

Utawala nchini Afghanistan, umeituhumu Pakistan kwa kuwaunga mkono wanamgambo ambao walisababisha vifo vya zaidi ya watu 95 katika mlipuko wa bomu wa kujitoa mhanga mjini Kabul.

Watu 158 wamejeruhiwa.

Unasema kwamba, shambulio hilo la jana Jumamosi, lililotekelezwa na kundi moja la wapiganaji la Haqqani, lililo na uhusiano mkubwa na lile la Taliban, na kuungwa mkono na Pakistan.

Utawala wa Afghanistan, sasa unaeleza kuwa shambulio hilo ni la kiwango cha mauwaji makubwa ya halaiki, dhidi ya binadamu.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Zaidi ya watu 150 wamejeruhiwa katika mlipuko huo

Siku zote Islamabad imekanusha madai ya aina yoyote ya kuyaunga mkono makundi ya wanamgambo yenye nia ya kuhujumu utawala wa Afghanistan.

Gari moja la dharura la kuwahudumia wagonjwa, ambalo lilikuwa limejazwa vilipuzi, lililipuka katika kituo cha usalama barabarani baada ya kusimamishwa na askari, katika Wilaya ya Jiji Kuu Kabuli kulikokuwa na idadi kubwa ya watu.

Image caption Ramani ya Kabul

Kwa njia ya taarifa, Rais wa Marekani Donald Trump, amelaani shambulio hilo, huku akitoa wito wa mbinu muafaka wa kupambana na kundi la Taliban.

Shambulio la sasa limetokea wiki moja tu baada ya Hoteli ya Intercontinental mjini Kabul kushambuliwa na watu zaidi ya 20 wakauwawa.

Mada zinazohusiana